Makonyeza
Member
- Feb 2, 2020
- 72
- 261
Kwanza nikukumbushe,nilishawahi kuandika,hakuna chuo wala darasa la kufundusha uchambuzi wa Soka.
Ukweli huu haimaanishi sasa kwamba kila mtu anaweza kuuzungumza Mpira na akaeleweka.
Na niweke angalizo muhimu,uchambuzi wa soka usichanganye na uhuru wa Maoni,maoni yanatolewa na mashabiki ambao wao huuzungumza mpira kwa namna isiyo rasmi (kishabiki).
Kila kituo cha habari huja au huibuka tu na mtu wanayemwamini wao kwa vigezo vyao kwamba anatosha kuwasaidia kuujadili mchezo husika,huyo tayari huitwa Mchambuzi wa masuala ya Soka.
Sasa hawa wachambuzi wamegawanyika makundi matatu ambayo ni:
1. Wachambuzi Weledi:
Hawa ni aina ya wachambuzi ambao huujadili na kuuzungumza mchezo wa soka kwa nukta zake muhimu. Hawa tegemea wakupe takwimu,historia, uwezo binafsi wa mchezaji mmoja mmoja na mwisho masuala ya kiufundi akijumuisha benchi la ufundi na timu nzima kwa ujumla wake.
Hawa huujadili mchezo wenyewe kwa ujumla tangu waamuzi mpaka chama cha soka na hawachagui pa kugusa,utawasikia wakijadili masuala ya soka kitaifa na hata kimataifa.
Mara nyingi aina hii ya wachambuzi kuwa ni wale waliokaa darasani na kuusoma mchezo wa mpira na kadha wa kadha zake.( sio kusomea uchambuzi).
Hawa humudu kuficha mapenzi na unazi wao kwa timu fulani.
Sifa yao ya ziada hawa hata linapokuja suala la sheria za soka wao hunyoosha mikono na kuwaacha au kuwaalika au kuwashirikisha wanasheria wataaluma kufanya kazi yao.
Lakini mwisho wa siku wao katika mijadala yao huzungumza hali halisi ya timu fulani na hata ikilazimu kusema mapungufu au udhaifu wa timu hiyo husema kwa staha na wakaeleweka.
Mfano wao namkumbuka Marehem Kashasha na swahiba yangu Ambangile.
2. Wachambuzi mashabiki:
Hawa ni wale wachambuzi ambao aidha waliucheza mpira wakiwa timu fulani au waliusoma mpira lakini wameshindwa kuficha mahaba na timu fulani.
Dalili zao hawa, ni taabu kuwasililiza coz hawataki kuizungumza hali halisi ya mambo kwa timu kadhaa,penye udhaifu ataficha au atasema kwa uwazi na kuzidisha chumvi.
Na kwenye ubora atasifu au atakejeli kwa kusema ni bahati,fluku au mpinzani alikuwa dhaifu utategemea anazungumzia upande gani.
Hawa pia uchambuzi wao hutawaliwa na hisia binafsi kuliko kuzingatia ile misingi na nukta muhimu za mchezo husika.
Timu ikipoteza atakwambia niliyajua haya, safari yao imeishia hapa...mara timu fulani ndio kubwa,...ooooh timu ile haina historia ya kufika pale. Utawasikia ...mechi hii ingekuwa timu ile....tungeongea mengine...,Yaani mazungumzo yao huwa ni Negativity tu shidi ya timu fulani.
Aina hii ya wachambuzi wao hujadili mpaka mikataba ya wachezaji na sheria ilhali hawana wajualo juu ya sheria
Hawa kwao timu fulani haina jema, ikishinda imebahatisha,ikifungwa imestahili. Yaani wao wanatangaza Chuki kwa timu fulani ya waziwazi.
Zaidi wamejidhihirisha tena bila haya wao ni wafuasi au mashabiki wa timu fulani.
Kaka yangu Jeff Yeye ndio aliweka wazi kabisa kwamba ni Mnyama.
Aina hii wengi wao ni waandishi wa habari za michezo, wanaotumia media zilizowaajiri kueleza hisia zao.
Lakini mwisho utawajua kwa matendo yao, wao hujipa 'mult task',hao hao hujiita wachambuzi,wao ni watangazaji na waandishi,bado wao ni mameneja wa wachezaji fulani na mashabiki kwa wakati mmoja.
3. Wachambuzi wasioeleweka:
Hawa,hawaeleweki kweli,haijulikani walicheza au walisomea soka.
Aina hii ya tatu ni wachambuzi ambao kutowaona wala kuwasikia popote zaidi ya kwenye kitandao ya Kijamii.
Aina hii ya wachambuzi wao huwezi kusikia akijadili Namungo wala Dodoma Jiji,sisemi kimataifa, wao hujadili timu za Kariakoo tu.
Ukiwasikiza wao hawajui misingi ya mchezo wa soka,zaidi hujadili kwa kutoa hisia zake kama dalali wa samaki ferry.
Hawa utawasikia tu,Yanga haina timu ya kufika makundi Caf,...mara Chama ni zaidi ya Pacome / Aziz mara mia[emoji1787],yaani mchambuzi eti anashiriki ubishani wa nani zaidi kati ya mchezaji fulani na mwingine.
Walisikika wakisema kwenye kundi hili Yanga ndo timu dhaifu kuliko zote, watapita Ahly na Beloudad...Yanga hatoshinda mechi hata moja,wao hawaoni taabu kujigeuza waganga wa kienyeji kuutabiri mchezo wa soka.
Yaani anaulizwa Yanga inakwenda kuwakabili Beloudad nini maoni yako... jibu lake ni 'Yanga ameshafungwa,hawawawezi Belouzadad...'[emoji1787]
Mara utasikia Yanga wanadanganyana...hawawawezi Mamelody watafungwa nyumbani na ugenini. Mara oooooh...Yanga wamemkosea heshima Kocha wao...
Hawa zaidi hujificha kwenye vimedia vya mitandaoni halafu hupost picha zao ili ajulikane ni yeye ndo kasema neno fulani. Negativity ndio msingi wa hoja na mijadala yao.
Huyu yeye anaonekana kwa tafiti zake anaamini kuisemasema vibaya timu fulani ndo itamuongezea watu kumfuata kwenye kurasa zake.