Aina tatu za watu katika maisha yako

Aina tatu za watu katika maisha yako

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
1. Watu Majani
2. Watu Tawi
3. Watu Mizizi

WATU MAJANI:
Hawa ni watu ambao wanakuja katika maisha yako kwa msimu tu. Huwezi kuwategemea kwa sababu ni dhaifu. Wanakuja kuchukua tu wanachotaka, lakini upepo ukija wataondoka. Unatakiwa kuwa makini na hawa watu maana wanakupenda mambo yakiwa sawa ila upepo ukija watakuacha.

WATU TAWI:
Wana nguvu, lakini unahitaji kuwa mwangalifu nao pia. Wanaachana wakati maisha yanakuwa magumu na hawawezi kuhimili uzito mwingi. Wanaweza kukaa na wewe katika baadhi ya misimu, lakini wataondoka hali inapokuwa ngumu zaidi.

WATU MIZIZI:
Watu hawa ni muhimu sana kwa sababu hawafanyi mambo ili waonekane. Wanakuunga mkono hata ukipitia wakati mgumu watakunywesha maji wakati wa kiu, watakulisha wakati wa njaa, na hawaguswi na msimamo wako wanakupenda hivyo hivyo. Sio watu wote unaokutana nao ni marafiki zako, watabaki na wewe. Ni watu wa aina ya mizizi pekee ndio watakaa bila kujali msimu [emoji818][emoji817][emoji1548].

Je, wewe ni mtu wa aina gani katika maisha ya wengine?

TAFAKARI[emoji188][emoji2827]
roots%20(1).jpg
 
Na Ni vizuri kukutana na kimbunga ili uweze jua matawi,majani na mizizi kwenye Maisha yako....
Frankly speaking Kuna sehemu kwenye Maisha ya watu nimesplay part zote tatu
Kuna sehemu nishakuwa majani
Kuna sehemu nishakuwa matawi na Kuna sehemu nishakuwa mzizi Mkuu.
 
Me washkaji zangu wengi naona ni watu majani,mnatafutana kwenye ulabu,ngono,sherehe na matumizi ya pesa...

Nimejaribu sana kuwakwepa/kubadiri marafiki lakini nashindwa yaan unamkataa mtu lakin bado utakuta amepaki kigari chake uwanjani pako...inakera sana.
 
Me washkaji zangu wengi naona ni watu majani,mnatafutana kwenye ulabu,ngono,sherehe na matumizi ya pesa...

Nimejaribu sana kuwakwepa/kubadiri marafiki lakini nashindwa yaan unamkataa mtu lakin bado utakuta amepaki kigari chake uwanjani pako...inakera sana.
Kama umeshawajua ni majani ishi nao kwa akili sana
 
Sitosahau vurugu za gesi Mtwara mjini kama utani duka langu lilivunjwa halafu mbaya zaidi ni siku sita tangu nirudi dar kufuata mali na kama ilivyokawaida nilikuwa nanunua mzigo kama tufanye wa elfu 10 kwa muhindi kule dar halafu ananikopesha wa elfu 5...

Kiukweli sitosahau yale maisha mpaka naingia kaburini kwasababu bidhaa zote zilibebwa dukani mpaka leo najiuliza waliwezaje kubeba nondo na bati ? Washkaji walinitenga sana na muhindi nae alipoona kimya kingi akaanza kudai pesa akaleta mpaka mwanasheria wake aisee noma balaa
 
Umenena vyema. Lakini hata huko kwenye mizizi, kuna matababa tofauti tofauti ya mizizi! Ipo mizizi itakayohimili mikiki mikiki kwa muda usio na kikomo, ipo ya muda wa wastani na na ipo ya muda mfupi. Mizizi bora ni ile imara isiyoathiriwa na dhoruba ya aina yoyote; haiwezi kung'olewa na upepo, hailiwi na mchwa wala kushambuliwa na magonjwa ya mimea. Hapa tunaongelea mizizi ya mti kama wa Mpingo, au kwa wenzetu wa nchi za Mashariki ya Kati wanasema mizizi ya mti wa Muerezi; mizizi hii ni imara na inahimili kila aina ya msukosuko. Lakini hebu niambie mizizi ya mpapai; je, unaweza kuitegemea?!
 
Back
Top Bottom