SoC04 Aina ya Viongozi, Wafanyakazi na Raia wa Kuipaisha Tanzania na Kuwa Kitovu cha Uchumi wa Africa Ndani ya Miaka 15

SoC04 Aina ya Viongozi, Wafanyakazi na Raia wa Kuipaisha Tanzania na Kuwa Kitovu cha Uchumi wa Africa Ndani ya Miaka 15

Tanzania Tuitakayo competition threads

The Student

New Member
Joined
May 30, 2024
Posts
3
Reaction score
1
UTANGULIZI
Swali la kuu la kujiuliza ni kuwa , Tanzania imekuwa na vizazi vingi tangu ilipojipatia Uhuru mwaka 1961 na kumekuwa na awamu takribani tano za Uongozi, kwanini adi leo hutujaipata Tanzania tunayoitaka na bado tunawaza kuwa na Tanzania tofauti na tuliyo nayo sasa?.

Mipango mbalimbali ya Kiuchumi imekuwepo tangu awamu ya Uongozi wa Baba wa Taifa adi awamu ya Uongozi wa sasa baadhi ikishindwa na nyingine kufanikiwa kufikia malengo. Tumebarikiwa Rasilimali nyingi, tuna ardhi ya kutosha, idadi ya watu tuliyonayo unaweza kuwa mtaji wa uchumi wa nchi yetu. Tatizo liko wapi adi leo tunatamani kuwa na Tanzania tofauti na tuliyonayo?.

Ili Tanzania iweze kufikia malengo ya kuwa kitovu cha uchumi wa Afrika ndani ya miaka 15 ijayo tunaitaji viongozi, wafanyakazi na raia wa aina hii;

VIONGOZI WANAOPATIKA KWA USHINDANI
Tumekuwa na viongozi wengi ambao wamepewa Mamlaka ya kuongoza Taasisi na Sekta mbalimbali za Serkalini kuanzia ngazi ya chini. Viongozi wengine wamekuwa na nyadhifa za uwakilishi wa raia katika ngazi mbalimbali za Utawala. Tangu tumejipatia Uhuru tumekuwa nao wakipewa dhamana ya kusimamia raia, wengine wakistaafu na wengine wakichukua nafasi na wengine kuhamia katika sekta na taasisi mbalimbali ili kuongeza ufanisi katika utendaji.

Mifumo tunayoitumia kama nchi kupata viongozi wenye maamuzi katika Taasisi na Sekta mbalimbali umekuwa na changamoto na kupelekea kulegalega kufikia malengo kama nchi katika Sekta na Taasisi husika. kama Nchi tumetumia mfumo wa uteuzi kwa muda mrefu na ndio umetufikisha apa tulipo na kutamani Tanzania nyingine yenye mabadiliko. Viongozi wengi wameshindwa kuwa wawajibikaji kwa wanachi kutokana na mifumo ya upatikanaji wao.

Ili kuwa na Tanzania itakayokuwa kitovu cha Uchumi wa Afrika ndani ya miaka 15 , ni muda sasa wa kuwa na nafasi nyingi za uongozi zinazopatikana kutokana na ushindani wa kitaaluma na uwezo kwa kuomba nafasi wanazotaka kuongoza.

Nafasi za uongozi katika taasisi zinazobeba uchumi wan nchi kama nishati, kilimo, madini na nafasi za uongozi katika ngazi mbalimbali ni vyema sana kupatikana kwa njia ya ushindani na utendaji wao utapimwa kwa mafanikio na hasara katika taasisi zao.

WAFANYAKAZI SERIKALINI KUFANYA KAZI KWA MIKATABA
Ili kuipaisha Tanzania kuwa kitovu cha Uchumi wa Afrika ni muda sasa kuanzisha mfumo wa wafanyakazi watakaofanya kazi kwa mkataba katika baadhi ya sekta na taasisi za serikali. Imwekuwa kawaida kwa mwajiliwa wa serkali kuanza kufikilia jinsi ya kusitaafa baada ya kuajiliwa kwani wengi wamekuwa wakiichukulia ajira ya serkalini kuwa ajira ya maisha. Hali ii imepunguiza sana ufanisi wa wafanyakazi serkalini katika sekta na taasisi mbalimbali. Mfumo wa kufanya kazi kwa mkataba utaleta ufanisi katika utendaji kazi kwni kila mfanyakazi atafanya kazi kwa kufata taratibu. Hii imefanikiwa Zaidi katika sekta binafisi ambazo zimepata mafanikio sana.

Mfanyakazi atatakiwa kufanya kazi kwa kipindi cha muda flani, pale anapoomba kuongezewa mkataba, utendaji wake utapimwa kwa mafanikio aliyopata katika nafasi aliyopewa. Mfumo huu unaweza kutumika katika nafasi za ajira serkalini. Huu mfumo wa kufanya kkazi kwa mkataba.

RAIA WAWAJIBIKAJI NA WENYE FIKRA PANA KWA MASLAHI YA NCHI
Ii kuwa na Tanzania itakayo kuwa kitovu cha Uchumi wa Afrika kwa miaka 15 ijayo, tunaitakuwa kuwa na raia wawajibikaji na wenyefikra pana kwa masilahi ya Taifa. Kwa miaka ya hivi karibu watanzania tumeshindwa kuwajibika ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi, kiasa na kitamaduni katika nchi yetu.

Raia ndio wanahusika moja kwa moja kuchagua viongozi, lakini tumepeleka ushabiki na masilahi ya vyama vyetu vya siasa mbele katika kuwachagua viongozi ata ambao tunajua hawawezi kutuletea maendeleo na kupelekea kupata viongozi wanaoshindwa kuwawakilisha vyema wanachi wao.

Maeneo mengi yamekuwa na changamoto za kimaendeleo ila kwakuwa raia tumejikita katika ushabiki wa vyama vya siasa tumesahau kupaza sauti juu ya changamoto mbalimbali zinazoyakabili maeneo yao.

Ni muda sasa raia kupadilika na kuwa na ujasili wa kuhoji maswala mbalimbali juu ya mustakabali wa Taifa. Tuna nafasi mhimu ya kuwapa mamlaka viongozi mbalimbali kupitia uchaguzi lakini tumeshindwa kuwasimamia kutokana na hofu, ushabiki wa vyama vya siasa. Ni muda sasa kuanza kuwahoji viongozi wetu juu ya kile walichofanya tangu tumewapatia nafasi wanazohudumu.

Hii itajenga uwajibikaji kwa viongozi wetu.
Kama raia wataendelea kuwachangua viongozi kwa kufata masilahi ya vyama vya itakuwa ngumu kufikia malengo, ila kama raia wataamua kuwachagua viongozi kwa kufata sera zao ambazo ni kuleta maendeleo itakuwa rahisi sana Tanzania kuwa kitovu cha uchumi wa afrika

Hitimisho
Tanzania tuitakayo ambayo ni kuwa kitovu cha uchumi wa Africa. Na hii itawezekana kwa kuruhusu baadhi ya nafasi za uongozi katika taasisi na sekta za serkali kupatikana kwa kuomba kazi na kufanyiwa usaili. Pia wafanyakazi wa serkali kufanya kazi kwa mikataba na kuwa na raia wawajibikaji ambao wataliangalia taifa katika jicho la kipekee na kuwajibika Zaidi kwa ajili ya vizazi vijavyo.
 
Upvote 1
Back
Top Bottom