Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Subalkheir ndugu zangu,
Baada ya andiko lililopita kufafanua aina mbalimbali za maneno (Soma hapa: Aina za maneno katika lugha ya Kiswahili) nikaona si vyema kuwaacha hewani. Kama nilivyoahidi kuja na ufafanuzi wa undani wa aina moja moja ya maneno, katika andiko hili tutaangalia aina za nomino. Twende pamoja hapa chini:
NOMINO
Nomino ni maneno yanayoeleza majina ya watu, vitu, mahali, hali, tabia au taratibu. Kwa mfano, Fatma, uvivu, nyumbani. kuna aina sita za Nomino ambazo nitazifafanua hapa chini.
AINA ZA NOMINO
1.Nomino za Kipekee
Nomino ambazo hutaja vitu vya kipekee. Nomino hizi hutaja kitu kwa kukitambulisha waziwazi kwa jina au majina yake kamili. . Majina haya huanza Kwa herufi kubwa ima iwe mwanzoni mwa sentensi au hata katikati. Nomino hizi hazina wingi.
- Mfano Kenya, Otieno nk.
2. Nomino za Jumla (Nomino za Kawaida)
Hizi ni nomino zinazotaja kitu bila kukitambulisha kwa jina lake halisi. Kwa mfano kama ni mji hatuambiwi ni Nairobi au Mombasa. Nomino hizi huanza kwa herufi ndogo isipokuwa tu zinapotokea mwanzoni mwa sentensi.
- Mfano wa nomino za kawaida, nchi, kitabu, mtu, nk.
3. Nomino za Jamii au makundi
Nomino za vitu vinavyotokea kwa makundi. Kila kundi hurejelewa kwa kutumia jina au nomino maalum.
- Kwa mfano, umati wa watu, tita la kuni nk.
4. Nomino za wingi
Nomino hizi hutokea tu kwa wingi. Haziwezi kugawika ili ziwe kitu kimoja kimoja.
- Kwa mfano, mazingira, maji nk.
5. Nomino dhahania, kufikirika
Majina ya vitu vya kufirika tu wala haviwezi kugusika, kuonjeka au kuonekana.Havina jumbo halisi.
- Kwa mfano, Malaika, Shetani, furaha, huzuni, wasiwasi nk.
6. Nomino za Vitenzi jina
Nomino zinazoundwa kutokana na vitenzi. Huundwa kwa kuongezewa kiambishi ‘ku_’ mwanzoni mwa mzizi wa kitenzi.
- Kwa mfano, kupika.
Credit kutoka vitabu:
- Kimani Njogu na Dorothy K. Nganje, kiswahili kwa vyuo vya ualimu: Jomo Kenyatta Foundation 2006
- Kimani Njogu, Alice Mwihaki na Aswani Buliba, Sarufi ya kiswahili: uchanganuzi na matumizi: Jomo Kenyatta Foundation 2006.
- Jamvi la Uhakiki wa Kiswahili

Mwakisyala Signed