Aina za ugali bongo

super black Boy

Senior Member
Joined
Oct 15, 2019
Posts
135
Reaction score
169
Habarini wanajamvi. Nilikuwa nahitaji kufahamu kuwa kwa hapa Tanzania kuna aina gani za ugali zinapatikana hapa bongo na aina zipi kati ya hizo zinapendwa sana na watu!!

Binafsi nafamu ugali wa sembe na Dona Je wewe mwenzangu unafahamu zipi na Je upishi wake ukoje??
 
Kuna mwingine unaitwa NTANDASA ni wa unga wa muhogo wakati wa kusonga moto unapaswa kuwa mdogo mdogo vinginevyo utatepeta
 
Unataka ugundue nini kwenye ugali?
Kuna ugali unaotokana na mahindi, ambapo kuna sembe na dona.
Pia kuna ugali unatokana na viazi, mtama, mihogo, ndizi etc.
mkuu kuna biashara nahitaji kuifanya so najaribu kufanya research watu wanapenda ugali wa aina gani kwa wingi
 
mkuu kuna biashara nahitaji kuifanya so najaribu kufanya research watu wanapenda ugali wa aina gani kwa wingi
Research ya ugali unaifanyia jf?
Kweli?
Hauko serious.
Sana sana ungesema unataka uifanyie wapi hiyo biashara yako ili iwe vizuri zaidi kusaidiwa.
Ungeweka wazi kwa mfano kuwa unataka kuifanyia Dodoma, kuna member wengi wanaifahamu Dodoma wanaweza kukufafanulia zaidi.
Sasa kama haujaweka wazi inakuwa ngumu.
Sababu ugali wanaokula kigoma (wanaotumia hasa) hauwezi kuwa sawa ugali wanaotumia Tanga.
Mfano Kigoma kuna ugali wa unga wa mhogo, ambapo sehemu nyingine ugali wa mhogo ni mtihani.
 
mkuu kama unaona mawazo yangu yapo pointless usiendelee kutema mapovu, na wala sijakulazimisha kucomment nini maana ya kuwepo JF au niambie vitu gani muhimu vya kufanya humu JF?? swali nililouliza ni jepesi sana so kama ww kwako huna chakusaidia piga kimya
 
kingine mkuu naelewa nachokifanya hapa hii ni sehemu kama ya source of data collection kama umesoma research kweli....hapa kupitia michango ya watu unapata kitu ambacho kinaweza kukujenga kwa namna moja ama nyingine hakuna aliyezaliwa anajua kila kitu mengine tunajifunza kupitia kwa watu na hayo tunayojifunza ndo yanachangia hata kupata kipato cha kujikimu kimaisha
 
Acha ujinga dogo,
yaani nakuelewesha, wewe unaleta upumbavu.
acha ujinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…