Aina za Uwekezaji wa Watanzania wengi hautupi nafasi kushindana huko Duniani

MURUSI

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
4,537
Reaction score
8,824
Uwekezaji unao fanywa na asilimia kubwa ya sisi Watanzania haitupi kuweza kushindana huko Duniani na mataifa mengine.

Tumekuwa na aina za uwekezaji ambazo sana ni kwa ajili ya Familia zetu na sio za kututambulisha Duniani au kusaidia nchi.

Chukulia mfano Mji kama Kahama, Ule ni mji una Mgodi mkubwa sana wa Madini na ule ni uwekezaji wa wazungu, Ukitoa ule uwekezaji wa Madini pale Kahama kinacho fuata ni Lodge, Car Wash, Guest House, Frame na kadhalika, hii ni kwa ajili sana ya sisi Wa Tanzania lakini hizi sio za sisi kutamba nazo nje.

Nenda Miji hata Geita kwenye uwekezaji mkubwa sana wa Mgodi pia wa Madini pale, baada ya Ule Mgodi sisi Watanzani hatuna uwekezaji wa kuja kuwapa chalange Wazungu.

Hii iko kwenye miji mingi sana, Ukienda, iwe Vijijini iwe mijini sisi Wazawa aina nyingi za uwekezaji wetu sio zile ambao zinakuja kuisaidia nchi mbele ya Safari bali kuja kitusaidia sisi Familia zetu mbele ya Safari.

Angalia wekezaji za Wazungu huku kwetu, angalia Wachina, angalja Wazungu na hata angalia Wakenya walio wekeza kwetu Tanzania.

Asilimia kubwa ya Watanzani tukiwa na na pesa ukisikiliza mawazo yetu na hata mimi mwenyewe ni kuwekeza either kwenye Usafiri, au kujenga Frame za Biashara au Lodge au Baa kubwa sana au Hoteli au Car Wash na kadhalika, ni Watanzania wachache mno mno utawasikia wanasema mimi nataka kuwekeza kwenye kilimona hizi pesa zangu, au nategemea kuwekeza kwenye viwanda au wekezaji zingine kubwa.

Tuwe wakweli wekezaji za Frame, Lodge, Baaa, Nyumba za kupanga, Mabasi na kadhalika hizi zina faida kwa sisi kama sisi ila hazina nafasi International.Hazitupeleki nje.

Nakaribisha challange.
 
Nakubaliana na wewe mkuu, asilimia kubwa ya watu wanashindwa kufikiri nje ya box...na ukiangalia biashara zenyewe hazina garantii yakusavaivu kwa wakati wote
 
Ni kweli. Nahisi uwekezaji mkubwa wa kimataifa ni lazima serikali itoe support, hata kwa ushauri au mazingira bora.

Kuna siku nilikuwa namsikiliza mmiliki wa kiwanda cha mafuta ya alizeti-Singida, alikuwa analalamika kodi ni nyingi sana.

Sasa, unajiuliza kwa nini fursa ya mafuta ya kupikia hatuichangamkii mpaka tunaagiza nje ya nchi?
 
Kuna nyanja kadhaa ambazo naona kabisa zinaweza kuleta faida kupitia soko la ndani tu.

Nyanja hizi ni kklimo cha mbegu za kutengeneza mafuta ya kupikia, pamoja na pamba kwa ajili ya kutengeneza nguo za kuvalisha zaidi wa watu miliom 55.

Huwa najiuliza, ni kwa ni kwanini bidhaa kutoka china inauzwa bei ndogo, kuliko bidhaa iliyotengenezwa hapa hapa Tanzania?
 
Fursa nyingine zinazokuja ni za percentage tu mpaka leo na watu wanaotaka bidhaa nyingine kutoka nchini lakini hawataka kuinvest ata kidogo sijui tatizo liko wapi au ndio kuogopa system.
 
Nadhani mitaji inasumbua, hao wawekezaji wanaowekeza kwenye hotel, lodge ,frame ndoo mtaji walio nao, hivi kiwanda ni mchezo ndugu yangu?
 
Ni kweli. Nahisi uwekezaji mkubwa wa kimataifa ni lazima serikali itoe support, hata kwa ushauri au mazingira bora.

Kuna siku nilikuwa namsikiliza mmiliki wa kiwanda cha mafuta ya alizeti-Singida, alikuwa analalamika kodi ni nyingi sana.

Sasa, unajiuliza kwa nini fursa ya mafuta ya kupikia hatuichangamkii mpaka tunaagiza nje ya nchi?
Yaani serikali ikushauri? Siku tutakapoondoa mentality ya serikali kweny equation ya mafanikio ndo siku tutakapotoboa. Haiwezekani kila kitu tufikirie serikali, serikali, serikali huu sasa ni uvivu wa kufikiri.
 
Kabisa
 
Kuna nyanja kadhaa ambazo naona kabisa zinaweza kuleta faida kupitia soko la ndani tu.

Nyanja hizi ni kklimo cha mbegu za kutengeneza mafuta ya kupikia, pamoja na pamba kwa ajili ya kutengeneza nguo za kuvalisha zaidi wa watu miliom 55.

Huwa najiuliza, ni kwa ni kwanini bidhaa kutoka china inauzwa bei ndogo, kuliko bidhaa iliyotengenezwa hapa hapa Tanzania?
China kula kwanza jua kunwa utitiri wa viwanda na pia wana pata sapoti na mazingira pia na ushindani ni mkubwa kiasi kwamba ubakuta wanatafuta faida ndogo sana.

Huku tuna tamaa kwenye kupanga bei, mtu anataka auze atatue matatizo yote
 
Kumbukeni kuwa Tanzania ilijengwa katika misingi ya kijamaa na Rais ndiye mmliki wa ardhi nchini. Hawa wawekezeji Wazungu wangeweza kupewa masharti ya kuwajengea wanakijiji nyumba bora self contained zenye maji na umeme kabla ya kuanza kuchimba dhahabu. Badala yake polisi wanapewa amri ya kuwafukuza wanakijiji na wanaokaidi kuondoka wanawekwa ndani.
 
Yaani serikali ikushauri? Siku tutakapoondoa mentality ya serikali kweny equation ya mafanikio ndo siku tutakapotoboa. Haiwezekani kila kitu tufikirie serikali, serikali, serikali huu sasa ni uvivu wa kufikiri.
Halafu tujiulize serikali ni nani?
 
Yaani serikali ikushauri? Siku tutakapoondoa mentality ya serikali kweny equation ya mafanikio ndo siku tutakapotoboa. Haiwezekani kila kitu tufikirie serikali, serikali, serikali huu sasa ni uvivu wa kufikiri.
Sijui kama unaelewa unachozungumza!

Serikali ndio inayo shape sekta binafsi. Serikali ndio mlezi.

Unazungumzia kilimo kwani ni nani kakwambia nchi hii watu hawajishughulishi na kilimo.

Mimi nitaendelea kusema, kila zao ambalo kwa kudra za Mungu lilionesha dalili za kutaka kumkomboa mkulima serikali imetumia nguvu kubwa sana kuliua.

Iko wapi Mbaazi, Pamba, katani, korosho, ufuta, kahawa ???

Juzi hapo NSSF wamechota pesa za wanachama kwenda kujenga kiwanda cha sukari. Wakulima wamelima, miwa imekomaa kiwanda hakijakamilika hawana msaada tena!

Mnawalaumu watu kufungua Car wash, lodge, guest house, Mpesa halafu mnataka kuitoa serikali kwenye lawama. Mnataka watu wafanye biashara zipi maana hizo biashara ndizo pekee serikali imeamua kutokuzifanya.

Hivi mmeshasahau ni mwaka jana tu serikali ilianza kufanya biashara kwa kufungua vituo vya mafuta ( TanzaOil ? ).

Mifano tu;
  • Yaani, Kwenye Clearing and forwarding wana TASAC,
  • Kwenye ulinzi wana SUMA JKT,
  • Ujenzi wana TBA,
  • Marking sasa hivi wana TBS
  • Angani wana ATCL
Ni biashara ipi sekta binafsi zifanye ili zisishindane na serikali zaidi ya hizo Mpesa, guest house, lodge n.k ???
 
Kumbukeni kuwa Tanzania ilijengwa katika misingi ya kijamaa na Rais ndiye mmliki wa ardhi nchini. Hawa wawekezeji Wazungu wangeweza kupewa masharti ya kuwajengea wanakijiji nyumba bora self contained zenye maji na umeme kabla ya kuanza kuchimba dhahabu. Badala yake polisi wanapewa amri ya kuwafukuza wanakijiji na wanaokaidi kuondoka wanawekwa ndani.
Mimi nyumbani Musoma, bahati nzuri kuna migodi mingi.

Kwa kawaida, wanakijiji huwa wanaosha marudio. Haya marudio ni mchanga ambao huwa una dhahabu kidogo na nyingi imeshaondolewa kwa kiasi kikubwa.

Lakini wanakijiji huwa wakiuosha tena wenyewe huwa wanapata angalau kiwango kidogo cha kuendesha maisha.

Mwanzoni huo mchanga ilikuwa wazungu wakishatoa dhahabu wanaumwaga ila ni ndani ya fence yao. Kwahiyo vijana wakawa usiku wanaruka fence wanaenda kuiba huo mchanga, kila siku ikawa ni purukushani na walinzi na polisi.

Sasa wazungu wakamshirikisha RC kwamba huu mchanga mbona wao hawana kazi nao, kama vipi uwe unamwagwa tu huko nje ili wananchi wachote.

Cha kushangaza huyo RC akawaambia kama shida ni wananchi kuvamia mgodi, yeye atapeleka FEED FORCE wasaidie ili kuimarisha ulinzi.
 
Hapa ndiyo tofauti unaiona kati ya mzungu na ngozi nyeusi. Mzungu atahakikisha maslahi ya watu wake yanakuja kwanza. Sisi yunakandamizana ili kumfurahisha mzungu.

Ninasikia kuna Rais wa awamu fulani aliulizwa tujenge nyumba za wanakijiji au tukujengee wewe binafsi hoteli South Africa, alichagua hoteli. Na bado hela za walipa kodi zitamjengea nyumba ya kustaafu.
 
Sijui kama unaelewa unachozungumza!

Serikali ndio inayo shape sekta binafsi. Serikali ndio mlezi.

Unazungumzia kilimo kwani ni nani kakwambia nchi hii watu hawajishughulishi na kilimo.

Mimi nitaendelea kusema, kila zao ambalo kwa kudra za Mungu lilionesha dalili za kutaka kumkomboa mkulima serikali imetumia nguvu kubwa sana kuliua.

Iko wapi Mbaazi, Pamba, katani, korosho, ufuta, kahawa ???

Juzi hapo NSSF wamechota pesa za wanachama kwenda kujenga kiwanda cha sukari. Wakulima wamelima, miwa imekomaa kiwanda hakijakamilika hawana msaada tena!

Mnawalaumu watu kufungua Car wash, lodge, guest house, Mpesa halafu mnataka kuitoa serikali kwenye lawama. Mnataka watu wafanye biashara zipi maana hizo biashara ndizo pekee serikali imeamua kutokuzifanya.

Hivi mmeshasahau ni mwaka jana tu serikali ilianza kufanya biashara kwa kufungua vituo vya mafuta ( TanzaOil ? ).

Mifano tu;

  • Yaani, Kwenye Clearing and forwarding wana TASAC,
  • Kwenye ulinzi wana SUMA JKT,
  • Ujenzi wana TBA,
  • Marking sasa hivi wana TBS
  • Angani wana ATCL

Ni biashara ipi sekta binafsi zifanye ili zisishindane na serikali zaidi ya hizo Mpesa, guest house, lodge n.k ???
Mbaazi, ufuta, korosho. Mikoa ya Lindi na Mtwara sasa hivi wanasaga Meno, hayo mazao serikali imeyaua
 
Mbaazi,ufuta,korosho..mikoa ya Lindi na Mtwara sasa hivi wanasaga Meno,hayo mazao serikali imeyaua
Hapo ndio ushangae. Serikali inataka watu wafanye biashara zipi?

Ndio maana watu wamekomaa na Bar, Grocery, Guest house, Mpesa.

Kila biashara kubwa ikionesha kuna pesa, serikali na yenyewe inataka kufanya.

Sasa hivi nasikia Parachichi zimeanza kuwa hot cake kwasababu zimepata soko huko China, ni suala la muda tu.
 
Hapa ndiyo tofauti unaiona kati ya mzungu na ngozi nyeusi. Mzungu atahakikisha maslahi ya watu wake yanakuja kwanza. Sisi yunakandamizana ili kumfurahisha mzungu.

Ninasikia kuna Rais wa awamu fulani aliulizwa tujenge nyumba za wanakijiji au tukujengee wewe binafsi hoteli South Africa, alichagua hoteli. Na bado hela za walipa kodi zitamjengea nyumba ya kustaafu.
Umasikini wa nchi yetu na watu wetu unaanzia kwenye roho za watawala.

Imagine, unakuta mtu ni Rais ambaye kwa kawaida anatakiwa mlezi na kuhakikisha kila mtu anafanikiwa, lakini anakuwa wivu kupindukia na hataki kuona mafanikio ya mtu.
 
Back
Top Bottom