Aina za Uwekezaji wa Watanzania wengi hautupi nafasi kushindana huko Duniani

Umasikini wa nchi yetu na watu wetu unaanzia kwenye roho za watawala.

Imagine, unakuta mtu ni Rais ambaye kwa kawaida anatakiwa mlevi na kuhakikisha kila mtu anafanikiwa, lakini anakuwa wivu kupindukia na hataki kuona mafanikio ya mtu.
Rais anatakiwa “Mlevi” au mie ndio sijala mchicha vizuri
 
Nakubaliana na wewe. Hata kwenye uwekezaji wa Pharmaceuticals Manufacturing bado mahitaji ni makubwa sana nchini na africa kwa ujumla.
 
Kama unaweza jenga lodge ya milion 900 hadi Bilion unashindwa kuanzisha kiwanda? Au kuwa na Farm kubwa? Mtaji sio shida,
Tatizo sio mtaji tu, nyakati nyengine tatizo ni kiwango cha ukubwa wa risk wa hauo mambo makubwa makubwa unayoona watu hawafanyi.

Kuna mtu ndio ni bilionea ama walau ni milionea, ila kuna biashara zina risk kubwa hata yeye mwenyewe haziingii kichwakichwa maana akifeli ni kwamba eidha kafilisika ama katetereka kwenye uchumi wake.

Mathalani uchimbaji madini, mtu anaweza katumia mamilioni, halafu sehemu alochimba ikawa haijarudisha mihela yote alotumia,

Kiwanda pia ni risk sana hata Dangote alikutana na misukosuko kwenye kiwanda chake cha cement huko Mtwara, si kwamba hana pesa, la hasha, ila huo ni uwkezaji wa mamia ya mamilioni, nazo zinaweza kupata hasara kama tu biashara ya mama ntilie inavyopata hasara, shida sasa ni kuwa hasara yake inakuwa ni pigo kubwa, hivyo watu wengine japo wanauwezo kwa kuwaangalia ila bado kuna sekta wao wenyewe hawazikurupukii tu, ndio maana uone Bakhresa na utaniri wake wote bado anawekeza kwenye ice cream kwasababu risk ya huko ndio anaona anaimudu, kuliko kutaka kuvaa mambo makubwamakubwa (japo pia kawekeza huko kwenye mabiashara ya marisk makubwa)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…