Aina za Vitenzi (T) katika lugha ya Kiswahili

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Wakuu salaam, tunaendelea na mada yetu ya aina za maneno katika andiko hili tutatazama vitenzi kwa upana wake. Tutaangalia dhana ya vitenzi kwa ujumla pamoja na aina zake. Twende pamoja tujadili. Ruksa kuongezea maarifa.

VITENZI
Vitenzi ni maneno yanayoarifu kuhusu jambo linalotendwa au kutendewa nomino. Vitenzi huwa na mzizi ambao kwamba ndio unaosimamia tendo lenyewe na mzizi huo huambatanishwa na viambishi ili kuleta maana inayokusudiwa. Kwa mfano, alipita.

A-li-viambishi awali

pit-mzizi

a- kiambishi tamati

AINA ZA VITENZI
1.Vitenzi halisi (Vikuu) (T)

Vitenzi hivi huonyesha kitendo halisi, kikubwa au muhimu kilichotendwa na mtendaji. Kwa mfano, mama anapika pilau.

2. Vitenzi visaidizi (Ts)
Ni kipengele cha neno au maneno kinachosaidiana na kitenzi kikuu ili kitendo kilichotendwa kifafanuliwe au kieleweke zaidi. Kwa mfano, mwalimu alikuwa anafunza hisabati.


3. Vitenzi vishirikishi
Vitenzi vinavyoshirikisha vitu kihali, kitabia au kimazingira. Kwa mfano:
  • Vedasto ni mvulana mtiifu.
  • Mwalimu wetu si mkali.
  • Yule ndiye mwanafunzi aliyeibuka wa kwanza.
  • Sisi tu mabinti wenye msimamo.

Vitenzi vishirikishi vimegawanyika katika aina mbili:

a) Vitenzi vishirikishi vikamilfu: Hivi vinaweza kuchukua viwakilishi nafsi au viambishi vya ngeli na pia viambishi vya wakati. Ni maneno kama, weza, kuwa, kwisha, kuja, taka, ngali, pasa, bidi, pata na kwenda. Kwa mfano:
  • Mtoto amekuwa kwa shangazi yake.
  • Kijana yule anapaswa kuwa hospitalini.

Vitenzi vishirikishi vikamilifu mara nyingine huweza kutokea kama vitenzi visaidizi iwapo vinatokea sambamba na vitenzi vikuu. Kwa mfano:
  • Mpishi alikuwa anapika.
b) Vitenzi vishirikishi vipungufu: vitenzi hivi haviwezi kuchukua viambishi vya wakati ingawa vinaweza kuchukua viwakilishi nafsi viambata au viambishi nngeli.kwa mfano:
  • Sharifa ni msichana mrembo.
  • Yule si mtoto mtukutu.
  • Gari li maegeshoni.
PIA SOMA:
Mwakisyala Signed

Credit kutoka vitabu:
- Kimani Njogu na Dorothy K. Nganje, kiswahili kwa vyuo vya ualimu: Jomo Kenyatta Foundation 2006

- Kimani Njogu, Alice Mwihaki na Aswani Buliba, Sarufi ya kiswahili: uchanganuzi na matumizi: Jomo Kenyatta Foundation 2006.

- Jamvi la Uhakiki wa Kiswahili
 
Nyumbani kuna wageni, kuna ni aina gani ya kitenz
 
Nyumbani kuna wageni, kuna ni aina gani ya kitenz
Neno kuna katika sentensi hiyo limetumika kama Kitenzi Kishirikishi Mkuu.

Sababu neno kuna halina hadhi ya kuwa kitenzi kikuu wala kisaidizi. Hili ni sawa na Sentensi hizi:
  • Juma si mrefu
  • Gali li matengenezoni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…