Aina za Viwakilishi (W) katika lugha ya Kiswahili

Aina za Viwakilishi (W) katika lugha ya Kiswahili

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Salaam Wakuu, tuendelee na somo letu pana la aina za maneno. Katika andiko hili tutasonga zaidi kwa kutazama kiundani Viwakilishi na aina zake. Twende pamoja.

VIWAKILISHI
Viwakilishi ni maneno yanayotumika badala ya nomino(vibadala vya nomino). Nomino husika huwa haitajwi katika sentensi. Kwa mfano, yule ni mtunzi mbuji wa mashairi.

AINA ZA VIWAKILISHI

1. Viwakilishi vya nafsi

Hivi ni viwakilishi vinavyosimamia viumbe vyenye uhai na hutokea ima katika nafsi ya kwanza, nafsi ya pili au nafsi ya tatu. (Zaidi Soma: Picha: Tazama mchanganuo wa nafsi katika lugha ya kiswahili na Kiingereza)

- Kwa mfano:
  • Mimi ni mwanafunzi katika chuo kikuu cha Masinde Muliro
  • Wewe ni mama bora.
  • Yeye ni ghulamu mtanashati.
Kuna aina mbili kuu ya viwakilishi vya nafsi:

a) Viwakilishi nafsi huru:
Hivi ni viwakilishi visivyohitaji kuongezewa viambishi vyovyote ili kujikamilisha. Navyo ni; mimi, sisi, wewe, nyinyi, yeye, wao.

b) Viwakilishi nafsi viambata (vitegemezi): Hivi ni viwakilishi vinavyotokea kama viambishi. Si maneno huru. Kwa mfano;
  • Nilikula chapati tamu sana .
  • Anatarajiwa kufika leo.
2. Viwakilishi vya ngeli
Hivi ni viwakilishi vinavyoonyesha kuwa nomino inayohusika imo katika ngeli flani. Kwa mfano:
  • Kilichopikwa ni chetu sote.
  • Yatafungwa jioni.
3.Viwakilishi vya sifa
Haya ni maneno ya sifa yanayosimamia nomino. Kwa mfano, Wakubwa wasubiri wadogo wale.

4.Viwakilishi vya A-Unganifu
Viwakilishi hivi hushirikisha majina mawili yenye uhusiano na hujengwa kwa kutumia A-unganifu. Kwa mfano, Wa zizini atachinjwa kesho.

5. Viwakilishi vya pekee
Haya ni maneno yalioundwa kutokana na mzizi ‘-ingine’, ‘-ote’, ‘-o-ote’, ‘-enyewe’ na ‘-enye’ na kutumika kama viwakilishi. Kwa mfano:
  • Lolote linakubalika.
  • Wenyewe waliingia nyumbani.
  • Mwenye kipaji cha kutunga mashairi amezawadiwa.
6. Viwakilishi virejeshi
Viwakilishi vinavyoundwa kutokana na kiambishi ‘o-rejeshi‘ au amba-. Kwa mfano:
  • Wanaokula ni wanangu
  • Nguo ambayo ulinipa ilinitosha sawa sawa.

7. Viwakilishi visisitizi
Hivi ni viwakilishi vinavyotumika kusisitiza nomino ambayo yenyewe haitajwi katika sentensi. Kwa mfano, Mwalimu anatumia Kiki hiki.

8.Viwakilishi vimilikishi
Hivi ni viwakilishi vinavyoonyesha umilikaji. Kwa mfano, Chake kimepotea.

9. Viwakilishi viulizi
Viwakilishi hivi hutumika katika swali. Kwa mfano, Nani ameenda sokoni?

10. Viwakilishi vya idadi
Hivi ni viwakilishi vinavyoonyesha idadi. Kwa mfano, Vinne vinatosha.

11.Viwskilishi vioneshi
Hivi ni viwakilishi vinavyoashiria kitu kinachozungumziwa. Kwa mfano, Yule alinisaidia sana.

Pia Soma:
Mwakisyala Signed
Credit kutoka vitabu:
- Kimani Njogu na Dorothy K. Nganje, kiswahili kwa vyuo vya ualimu: Jomo Kenyatta Foundation 2006

- Kimani Njogu, Alice Mwihaki na Aswani Buliba, Sarufi ya kiswahili: uchanganuzi na matumizi: Jomo Kenyatta Foundation 2006.

- Jamvi la Uhakiki wa Kiswahili
 
Back
Top Bottom