Aina za Wapenzi Hatari kwenye mahusiano

Aina za Wapenzi Hatari kwenye mahusiano

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
AINA ZA WAPENZI HATARI KWENYE MAHUSIANO...

1: Mpenzi mtangazaji--> Kila mnacho fanya yeye anaenda kusema kwa marafiki/ndugu/mitandaoni.

2: Mpenzi mtazamaji: Hana afanyalo, hana future, yupo yupo tu kazi yake ye kutazama na kusimulia ya wenzie wala yake hayawazii.

3: Mpenzi msikilizaji: Chochote watakachosema marafiki zake, yeye anafata. Lolote atakalo lisikia yeye anakuja kukuhukumu hata kama hana uhakika.

4: Mpenzi gogo🔞: Hana jipya kwenye bed, unashughulika wewe tu, yeye kazi yake kutoa miguno tu wala hakupi hamasa ya kufika kileleni. Hamna chochote kile anachofanya kwako, hashughuliki na lolote lile litakalo kupa furaha.

5: Mpenzi jini: Haku tafuti hadi akiwa na shida zake, zako wala hana mpango nazo. Anapenda umtimizie kila atakacho, tena ukishamtimizia hana mpango tena na wewe.

6: Mpenzi fisadi: chumaulete, muhujumu uchumi, anakugeuza kama kitega uchumi. Akitaka hata kwenda choon utasikia ''Baby naomba hela ya maji ya kutawazia''. Una muhudumia kila kitu lakin bado hana shukran kama tumbo la Kazora. Hana mawazo chanya, hawazi maendeleo, hata pesa uliyotunza kwaajili ya biashara utakuta kaitumbua yote. Unayajua majukum yako lakini yeye halitambui hilo.

7: Mpenzi pasua kichwa; Yeye ni wa kukupa stress tu, hana muda wa kukuliwaza wala kukudekeza, ukirudi home salamu "Umeniletea dera langu"??? Ndani kelele tu, yani ana gubu mpaka kero.
 
Ongeza mpenzi mchunguzaji
JamiiForums1509185792.jpg
 
Emmanuel Kasomi umesahau kusema wapenzi wa kike.....(sifa tajwa hapo juu zina elekea kwa sisi wadada)

Ila tunajisahau sana.....sisi ni dada zetu, wadogo zenu, mama zenu, pia watoto zenu.....hizi tabia tunazipata wapi kama sio kwenye hii hii jamii mliokuwepo na nyie wanaume.

Tupendane , tufundishane, na tuvumiliane....
tupunguze kunyoosheana vidole.
 
Emmanuel Kasomi umesahau kusema wapenzi wa kike.....(sifa tajwa hapo juu zina elekea kwa sisi wadada)

Ila tunajisahau sana.....sisi ni dada zetu, wadogo zenu, mama zenu, pia watoto zenu.....hizi tabia tunazipata wapi kama sio kwenye hii hii jamii mliokuwepo na nyie wanaume.

Tupendane , tufundishane, na tuvumiliane....
tupunguze kunyoosheana vidole.
Asante Sana D1vine kwa nyongeza hizo pamoja na ushauri
 
Back
Top Bottom