Air Bus Yapata hitilafu: Nani awajibike?

Gembe

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2007
Posts
2,483
Reaction score
164
Heshima mbele,

Kwa tarifa ambazo nimezipata mchana wa leo ni kuwa,ile ndege yetu ya Air bus jana ilipata itilafu na kushindwa kutoa matairi kabla haijaruka kwenda Mwanza ,na hivyo kuwalazimu ATCL kuhairisha safari ya mwanza kwa jana.Hii iisabbisha abiria wote waliokuwa wakisubiri ndege hiyo jijini mwanza na Kilimajaro kupangishiwa nyumba katika hotel za kitalii.

Maswali ya kujiuliza ni kuwa,

1.Je zile nege zilikuwa Mpya ?

2.Gharama ambazo ATCL inainghia kila siku kuweka watu hotelini ni nani analipa.

Kwa taarifa ambazo nimezipata toka kwa wafanyakzai wa ATCL ni kuwa ATC imebakiza ngege mbili tu kwa hivi sasa.

Hivi kwanini Mataka asijiuzuru?tumepiga kelee sana imetosha..sasa tuwaloge tu kama inawezekana ii waachie ngazi.Tumeumia pesa nyingi kukodi ndege mbovu sana..Mkuu invisible naomba uirudishe ile thread ya Ndege hizi..Mwanakijiji was very right at the begining
 
Hata safari za comoro zomesimamishwa kwa sababu shirika la ndegela tanzania linadaiwa pesa fulani huko pesa hizo ni kutokana na shirikala community airways ambao walikuwa wameingia mkataba fulani na kampuni za huko komoro ambao malipo yake yalikuwa yanatolewa na atcl
 
Nafikiri mkuu unatakiwa kufanya uchunguzi wa kina kabla ya ku-post. Mimi binafsi mkasa mzima unaniacha hoi, kwa kuwa najua kuwa tairi huchomolewa kabla ya kutua na si kabla ya kuruka.

May be kulikuwa na hitilafu kwenye hydrolic system ambayo hutumika ku-eject matairi wakati wa kutua ama kuyakunja ikisha-take off.

N'way kunaweza kukawa na matatizo lakini tupe kisa kamili kwani hilo ni shirika la umma na si la Mataka.
 
Sichangii tena kuhusu ATCL... tumeimba hawakucheza, tumepiga kelele hawakushtuka na tumewaita hawakuja!
 

Hili dege si ndio lile mkuu fulani alinipenyezea data kuwa lilikuwa "juu ya mawe" huko Venezuela, ambako ilipopatikana tenda ya kutafuta ndege wajanja wakachangamka likakarabatiwa chapchap tukaletewa!
 
Jamani mnataka wakale wapi? wakale polisi wakati wana ofisi na mnawalipa mishahara kiduchu, wamelikodisha dege bovu wakati wanajua kuwa wenye nayo wanaendelea kudai pesa hata kama halitatembea.
 
afadhali mmesema, mimi na atcl basi, ndege air bus ilikuwa imtelekezwa uwanja wa ndege wa carcass venuzuela, leo inatua na kuruka viwanja vya bongo?
 
Kwani sheria ya SUMATRA inyotaka vyombo vya kubebea abiria vilivyozidi miaka mitano visiingizwe nchini haihusu usafiri wa ndege????????????????
 
Duh! Hii inatisha. Hivi kweli hawa watu hawana uchungu na maisha ya watanzania wenzao? Yaani itabidi tuache kabisa kusafiri na ATC. Mimi nilidhani kama tukilisupport shirika "letu" basi tungeweza kulibadilisha kiuchumi, lakini la. Halafu nimesikia pia kwamba hiyo ndege "imekuja" na rubani wake ambaye amepangishiwa chumba kwenye hoteli ya Movenpick kwa muda wote wa mkataba!!!
 
Last edited:

MAJIBU YA MASWALI YAKO:
1. Ndege hizo hazikuwa mpya

2. Gharama za kuweka watu hotelini zinalipwa na ATCL yenyewe.

3. Mataka hawezi kujiuzulu kwa sababu nyingi tu; moja ni kuwa hajaona kama kuna makosa ameyafanya; mbili ana ubavu wa kufanya hivyo
 
Nimeshukuru sana kwa kukumbuka makala ya mwanakijikiji Especially wakati Waislam wenzetu walipokwama kwenda HIJJA MAKKA.Alijadili sana Uzembe wa mkurugenzi wa ATCL Lakini kama kawaida yao huwa wanajiona kama hawana makosa.YAANI ATCL ni kama imekufa vile sasa hivi HAINA TOFAUTI SANA NA RELI YA KATI.Wacha Rais wetu awe na ndege yake maana nahisi angekataa kupanda za SHIRIKA LA NCHI YAKE ANAYOIONGOZA.Hivi wadau mbona hawa watu hawajifunzi HATA KWA MAJIRANI ZETU WA KENYA??????????
 
Yaani itabidi tuache kabisa kusafiri na ATC. Mimi nilidhani kama tukilisupport shirika "letu"

HAPANA HIYO SII SOLUTION,TUNAITAJI KUSUPPORT ATC MKUU KADRI TUWEZAVYO...
KAMA WEWE UTAKATAA KUSUPPORT NATUMAINI WENGINE WATAFANYA KAMA WAZALENDO..TUFANYE KWA AJILI YA NCHI YETU!!!LEO KESHO LIKIFA NI WATANZANIA TUNAUMIA NA SI MATAKA NA WENGINEO ......HILO NI WAZO

PILI:NAZANI KUNA WAKATI INABID TUWE WAZI,JUZI BRITISH IMELALA NASIKIA HAPO AIRPORT HAKUNA ALIEPIGA KELE,AIR QATAR NAYO IMELALA HAKUNA ALIEPIGA KELE,,KWELI TUWASAIDIE ,ILA KW MAELEZO YAKO HAPO NAHISI HILOO NI SWALA LA TECHN PRBL AMBAYO HUZIKUMBA KILA NDEGE..NA NI LAZIMA ICHELEWE FOR MAINTANANCE, AMA LIPI BORA ICHELEWE AU IRUKE WATU WAFE?????

basi tungeweza kulibadilisha kiuchumi, lakini la. Halafu nimesikia pia kwamba hiyo ndege "imekuja" na rubani wake ambaye amepangishiwa chumba kwenye hoteli ya Movenpick kwa muda wote wa mkataba!!!
 
Kama ukiangalia hoja moja iliyowahi kuletwa hapa:

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/19400-atcl-je-sasa-inaandaliwa-makazi-ya-kudumu.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/17890-atcl-gets-lease-fly-again.html

https://www.jamiiforums.com/jf-exclusive/1207-atcl-another-richmond.html

Utagundua kuwa wadau walishaona mapema upupu huu. Suala la rubani hilo pia tulishaliona mapema, nashukuru kwa kukumbushia hili kwani watatambua kuwa hatujasahau. Majuzi nikiwa Mwanza nililazimika kubadili flight baada ya kuelezwa mikasa inayolikumba shirika letu hili.

Wanaolimaliza shirika hili ni watanzania wasiokuwa na uzalendo. We strongly stand against them!
 
Yaani itabidi tuache kabisa kusafiri na ATC. Mimi nilidhani kama tukilisupport shirika "letu"

HAPANA HIYO SII SOLUTION,TUNAITAJI KUSUPPORT ATC MKUU KADRI TUWEZAVYO...
Mkuu umenena vema, lakini hawa jamaa hawaamki bila watanzania kuchukua hatua za kuwaonesha kuwa wanachofanya kinakera.
KAMA WEWE UTAKATAA KUSUPPORT NATUMAINI WENGINE WATAFANYA KAMA WAZALENDO..TUFANYE KWA AJILI YA NCHI YETU!!!LEO KESHO LIKIFA NI WATANZANIA TUNAUMIA NA SI MATAKA NA WENGINEO ......HILO NI WAZO
Mkuu uzalendo watu tunao sana, binafsi napenda kuunga mkono kila jitihada za kuliinua taifa letu kwa kuingiza kipato na nimekuwa nikitumia ATC kwa safari zangu ndani ya nchi. Tatizo kubwa ni kuwa hawa jamaa wamelala au wanatuona vilaza kiasi flani.
Mkuu udhaifu wa wengine tusiuhalalishe kuwa ni kawaida. Lazima tuhakikishe ubora zaidi ya wao. Kwanini tuwe kama wao? Hapana, hakuna anayetaka kupanda ndege mbovu labda kama hajui ukiwa angani unakuwa nusu marehemu... Sasa ukizidisha kuwa nusu ukafikia "Robo tatu" huoni inakuwa balaa zaidi?
 
Hata kununua engine Mataka imekushinda ndege imepaki mwanza leo mwezi wa ngapi madeni madeni kila mahali priority kuwalipa wenye mahoteli kwanza mnaolaza abiria hiyo airbus ikiharibika ndio basi hakuna ndege nyingine loo aibu
 
Mama Subi na wengineo,

Soma hizi issues tatu mkumbuke tulikoanzia:


Kisha:


Chanzo: https://www.jamiiforums.com/jf-exclusive/1207-atcl-another-richmond.html#post12789

Na baadaye hivi:


Source: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-inaandaliwa-makazi-ya-kudumu.html#post305085
 

Hii mbona imekaa ki-rivasi bingwa wa rivasi! Ndege itashindwa vipi kutoa matairi ikiwa on the ground wakati inasimamia matairi hayo hayo?
 
Kwani sheria ya SUMATRA inyotaka vyombo vya kubebea abiria vilivyozidi miaka mitano visiingizwe nchini haihusu usafiri wa ndege????????????????
Kumbe SUMATRA wanahusika na usafiri wa anga!!! maajabu ya dunia haya...

Mimi ninavyofahamu... SUMATRA ni nchi kavu na majini... na Huko Angani ni TCAA.
Mungu Ibariki Tanzania
 
Kumbe SUMATRA wanahusika na usafiri wa anga!!! maajabu ya dunia haya...

Mimi ninavyofahamu... SUMATRA ni nchi kavu na majini... na Huko Angani ni TCAA.
Mungu Ibariki Tanzania

Kuna taasisi inaitwa Tanzania Civil Aviation Authority (TCAA), hawa ndio hasa wanahusika na masuala ya usafiri wa anga
 
Kumbe SUMATRA wanahusika na usafiri wa anga!!! maajabu ya dunia haya...

Mimi ninavyofahamu... SUMATRA ni nchi kavu na majini... na Huko Angani ni TCAA.
Mungu Ibariki Tanzania
Niulipouliza nilikuwa najua kuwa SUMATRA wanahusika na masuala ya nchi kavu na majini. Lakini nia na msisitizo wangu ulikuwa kuhusu uingizaji wa vyombo visivyozidi miaka mitano nchini. Ndege ni chombo cha usafiri. Kwa nini hakihusiki na sheria hiyo? "Risk" ya ndege iliyozeeka ni kubwa kuliko basi la abiria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…