Air Tanzania na huduma mbovu ya usafirishaji wa Parcels/ Mizigo

Air Tanzania na huduma mbovu ya usafirishaji wa Parcels/ Mizigo

Consultant

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2008
Posts
11,503
Reaction score
20,892
Nilitumiwa parcel moja kutoka Dodoma kuja Dar last month. Suprisingly, akapewa mtu mwingine anayeishi Chanika. Yaani ilichukua zaidi ya masaa 28 kuipata ile parcel na ilinilazimu mimi kudrive kumfuata alipo.

Nimetuma box dogo tu lenye documents kwenda Bukoba tangu tarehe 30 December. Cha ajabu, haijafika mpaka muda huu. Kitengo kinachohusika na Cargo pale Airport hawanipi majibu yaliyonyooka. I am very disappointed kwa huu uzembe uliokithiri. Ningetuma ile parcel kwa Bajaji ingekuwa ishafika muda huu.

Itabidi turudi kwa DHL tu sasa na tulipe zaidi kwa huduma bora!!😕
 
Sekta za umma ni shida mno. Ingekuwa private tayari mtu angekuwa fired
 
Consultant, Sekta za umma uendeshaji wake unakera sana. Hakuna mradi serikali yetu inaweza ikaendesha watu wakafurahia.
. Harafu eti hawa wanataka kuua other airlines ili wabaki peke yao. Ukiingia kwa website yao ofisi nyingine za mikoani hazina information on telephone numbers. Hata hizo ofisi zenye namba, namba zilishafungwa na TTCL kwa sababu ya madeni. Hatari sana
 
Nilpanda ndege Bukoba bag langu wakalishusha Mwanza nikalipata baada ya siku mbili.
Yaani kwa huduma ATC ni moto wa kuotea mbali kama siyo karibu Bro
 
Nilpanda ndege Bukoba bag langu wakalishusha Mwanza nikalipata baada ya siku mbili.
Yaani kwa huduma ATC ni moto wa kuotea mbali kama siyo karibu Bro
Tarehe 23 Dec 2019, walighairisha ndege ya Dar Mwanza mara kadhaa wakati watu wakiwa airport na walishaboard wakashushwa .. tarehe 30 Dec 2019, ndege ya sa 10 na dk 40 ikapelekwa saa 1 usiku, na ikabadilishwa tena hadi saa 4 usiku... yaani hawa jamaa kama unaunganisha ndege wala si wa kuwaamini kabisa... au kama unawahi apointment au mkutano wallah huwezi... HAIWEZEKANI KILA ROUTE IWE NA SHIDA
 
Back
Top Bottom