Air Tanzania yaanza rasmi safari zake Mtwara - Dar

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limezindua huduma za usafiri wa ndege za shirika hilo mkoani Mtwara ambapo ndege hizo zitakuwa zikifanya safari za Dar es Salaam-Mtwara mara tatu kwa wiki.

Akizungumza Februari 17, 2025 wakati wa uzinduzi wa safari za ndege hiyo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Arif Jihann, amesema Mtwara ina nafasi muhimu katika uchumi wa Tanzania kutokana na rasilimali zilizopo.

Ameongeza kuwa kurejeshwa kwa safari za usafiri wa anga kupitia ndege za Air Tanzania kutachochea ukuaji wa sekta ikiwemo uwepo wa nishati ya gesi, uvuvi, kilimo biashara na utaliii wa fukwe.

Naye Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara Jordan Mchami amesema kutokana na kuwepo kwa gharama ndogo za nauli kwenda na kurudi kati ya Mtwara na Dar es Salaam ambayo ni shilingi 199,000, kutasababisha kuongezeka kwa abiria watakaotumia usafiri huo.

“Hapo awali tulipokuwa na shirika moja la ndege nauli ilikuwa Shilingi 300,000 mpaka zaidi ya 400,000 maana yake ni hakukuwa na ushindani”, amesema Mchami.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara amesema uamuzi wa kurejeshwa safari hizo siyo tu zitafungua milango mipya kwa Mtwara kama kitovu muhimu cha biashara, uwekezaji na utalii lakini pia zitatatua changamoto kubwa za usafiri wa anga ambazo wakazi wa Mtwara na mikoa jirani wamekuwa wakizikabili kwa muda mrefu.

"Kurejea kwa Air Tanzania hapa Mtwara kumerahisisha urahisi wa safari na mmeweka nauli punguzo maalum la Shilingi 199,000 kwa safari ya kwenda na kurudi, amesema Mwaipaya.

Kwa upande wao baadhi ya wananchi wanaotumia usafiri huo akiwemo Asina Nanyanga amesema ujio wa ndege hiyo Mtwara umekuwa ni fursa kubwa kwao kwasababu utarahisisha upatikanaji wa huduma hiyo kwa urahisi zaidi.
1739798113262.png
 
View attachment 3239232
Hamna tena short break pale nangukukulu
 
Back
Top Bottom