newmzalendo
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 1,385
- 568
Habari wana jamii forum,malipo ya kupiga simu za Airtel kwenda Airtel kuanzia saa tano usiku mpaka saa kumi na mbili asubuhi ni robo shilingi kwa sekunde,naomba kwa ambae anadhani alikatwa pesa zaidi anipatie namba yake na tarehe uliyopiga simu ili niweze kuangalia na kushugulikia suala lake na kumpatia feedback, I will be more than willing to assist you and provide any clarification if need be.
Wewe ni Airtel?
Kaka hawa jama ni waongo sana na wanaboa atakua ni mmoja wao na kaingi JF baada ya kuon hii ishu. Ngoja niweke thread nyingine ya AIR PATEL!
Habari dugu,ndio mimi ni mfanyakazi wa Airtel naomba nikusaidie tafadhali kuhusiana na hili suala lililoletwa na mwana jamii mwenzetu,viwango vya kupiga simu Airtel kwenda kuanzia saa tano usiku 11pm mpaka saa kumi na mbili asubuhi 6am ni robo (1/4) shilingi.
Wewe ni Airtel?
Kaka hawa jama ni waongo sana na wanaboa atakua ni mmoja wao na kaingi JF baada ya kuon hii ishu. Ngoja niweke thread nyingine ya AIR PATEL!
Inasikitisha sana kuona kila kampuni inapoingia nchini inakuwa na lengo la kuvuna chee bila jasho. Moja ya wizi wa waziwazi wa hii inayoitwa Airtrel (Zamani Zain) ni hii promosheni yao ya Jirushe ya dakika 15 na kwa Tsh 250 na Dakika 30 kwa 500. Jamaa hawa hutuma msgs za kukuhamasisha ujiunge na Jirushe ya Dakika 15 kwa kutuma msg kwenda 155558 na ukituma tu wanakutumia msg ya kukupongeza na kukueleza namna ya kupiga simu na kuuliza salio la msg na simu. Lakini kinyume chake hutokea. Kila upigapo wanaendelea kukukata fedha na kukutumia msgs za gharama ulizotumia kwa mazungumzo hadi inapofika muda wa mwisho wa kujirusha. Mimi nimeshajaribu zaidi ya mara kumi na zote nimeliwa hela mara ya mwisho ni leo hii. Tunaomba Tume ya mawasiliano iwabane vibaka hawa. Kwa juu juu, shilingi 250 zinaonekana ndogo; lakini inafahamika kwamba mitandao hii ina watu zaidi ya milioni tano, sasa tafakari endapo waliohamasika kama mimi na kuibiwa 250 hizo tutafikia milioni moja kwa siku. Wahuni hawa watakuwa wamekomba milioni 250 kwa mpigo kiulainiii!Habari ndugu wana Jamii forum,
kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu katika kituo chetu cha huduma kwa wateja namba 100, au unaweza kututumia barua pepe helpdesk@tz.aitel.com ili tuweze kukuhudumia katika suula hili la mpango wa malipo wa robo shilingi kwa kupiga simu za Airtel kwenda Airtel kunazia saa tano usiku mpaka saa kumi na mbili asubuhi (11;00pm - 06;00am) au unaweza ukanipigia simu kwenye namba 0787 500 500 ili nikuhudumie.
Pia kama una swali lolote,au unahitaji maelezo yoyote kuhusiana na huduma zetu tafadhali wasiliana nasi na tutakuhudumia.
Ahsante.