Airtel 5G Unlimited Internet

mimi nipo kwenye halotel M2M, Yani nitateseka balaa nikiingia tuu meeting inakata, ila instagram haina shida inafunguka vizuri tuu,wakati mimi nimeisajali kwa ajili ya kufanya kazi na sio kuperuzi instagram na youtube. Kwa kweli Tanzania sijui tuna tatizo gani?
 
Mkuu, hiyo 10Mbps kwa nini uliamua ku upgrade? Ilikuwa haitoshi kwa matumizi yako?
 
Kwa mfano ukiacha kulipia mwezi mmoja au zaidi kuna shida?

Assume nimenunua router na kuunha cha 70 then kikaosha mwezi unaofata sihitaji internet labda Moka mwezi mwingine je inakuwaje
 
Kwa mfano ukiacha kulipia mwezi mmoja au zaidi kuna shida?

Assume nimenunua router na kuunha cha 70 then kikaosha mwezi unaofata sihitaji internet labda Moka mwezi mwingine je inakuwaje
Kwa Airtel haina shida, ila kwa voda hilo ni deni watakudai.
 
Kwa mfano ukiacha kulipia mwezi mmoja au zaidi kuna shida?

Assume nimenunua router na kuunha cha 70 then kikaosha mwezi unaofata sihitaji internet labda Moka mwezi mwingine je inakuwaje
Nikama utumiavyo laini zingine tu kwamba hujalipia hupati huduma.Ila kama hutolipia kwa miezi kadhaa watakuchukulia hatua zingine ilo kwakweli sijui.
 
Kiongozi, hebu nipe elimu manake miluzi inanipoteza. Kwa jinsi watu wanavyoongea ni wazi wanachotoa sio unlimited bali wanatoa kiasi fulani cha GB na baadae ku-apply throtting pale GB ulizopewa zinapoisha. Je, unaweza kuwa na idea kwa ile plan ya 70K inaweza kuwa ni GB ngapi? Au hiyo ya kwako ni plan ipi hasa?
 
Plan ya 70K ni 10Mbps hakuna kipimo cha MB.

Maana yake ni unlimited yenye speed ya 10Mbps na sio kuwa unatengewa MB kadhaa kwamba zikiisha katikati ya mwezi basi inabidi ulipie tena.
 
Kama unlimited Upo Pande za Mombasa, bombambili, gongo lamboto

Tuchekiane wazee nahitaji kushusha files Large Kidogo Bei tunaelewana
 
Mi natumia tigo 5g speed inashuka mpaka 1mbps nimejuta wakata walisema speed 20mbps
 
Plan ya 70K ni 10Mbps hakuna kipimo cha MB.

Maana yake ni unlimited yenye speed ya 10Mbps na sio kuwa unatengewa MB kadhaa kwamba zikiisha katikati ya mwezi basi inabidi ulipie tena.
Dah! Afadhali manake nimefuatilia TTCL hadi nimechoka. Hakuna namna itabidi Tigo Postpaid niwapige chini na 80GB zao! Nawe Mkuu Kanungila Karim, bakini na Fiber Internet yenu ya TTCL
 
Airtel ni walaghai, baada ya kuuza tu modem twao, wamebadili ma bundle na kurudi mle mle, nimeshakivunja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…