Airtel huduma kwa wateja ni janga la kitaifa

mdudu

JF-Expert Member
Joined
Feb 6, 2014
Posts
7,013
Reaction score
10,000
Ndugu Wanajamvi,

Nimepata tatizo kuhusiana na Airtel Money siku ya ijumaa, na nipo kijijini. Lakini kila nikipiga huduma kwa wateja namba 100 ili niwaeleze tatizo langu hawapatikani.

Chakujiuliza ni kwamba, inawezekanaje mitandao mkubwa wa mawasiliano wakakosa namba ya simu ya kuwahudumia wateja?
 
Hawa jamaa ukipiga namba 100 hawana option ya kuongea na mhudumu.

Mimi nikiwa na shida huwa nawafuata Inbox yao ya Facebook Page
 
Pole, usitumie neno "janga" tena la "kitaifa" unajua jambo/ kitu kuwa janga tena la Taifa linakuwaje kuwaje? na ili liwe janga hadi Rais atangaze hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…