ACCOUNT FULL
JF-Expert Member
- Sep 24, 2012
- 1,995
- 389
Kabisa!! Sasa badala ya Airtel Money wawe fear, wao wanafanya maamuzi ya upande mmoja!! Haina maana kuwa wakala wa Airtel Money kama wanachukulia mambo rahisi hivi.Bro labda jamaa hao watakuwa wametuwa AIRTEL kwenda kuwanyoosha MAWAKALA. Baya zaidi, mawakala hawawezi kujua mara moja kama wanapigwa
Hapa ni analia anatamani afunge tu Ofisi yenyeweMaskini wakala💔
Mpe poleHapa ni analia anatamani afunge tu Ofisi yenyewe
kwani Terms and Conditions za wakala zinasemaje kuhusu hili?Kuna mdada anayeishi Tabata, ambaye aliwasajiliwa laini na mawakala wa Airtel waliokuwa wakipita mitaani.
Bila yeye kujua, mawakala hao walifanya SIM swap kwenye laini yake. Baadaye, wale waliosajili laini hiyo waliitumia kwenda kwa wakala wa Airtel Money na kutoa pesa kwa njia halali—simu ikiwa na laini sahihi, namba ya siri ikiingizwa, na pesa ikitoka kama kawaida.
Wakala, bila kujua kuwa anahudumia tapeli, alitoa pesa taslimu.
Mdada aliyekuwa mmiliki wa laini hiyo alikuja kugundua kuwa pesa zake zimetolewa alipokea ujumbe wa uthibitisho.
Alipopiga simu Airtel Money, fedha zake zikarudishwa bila hata wakala aliyetoa pesa kuarifiwa. Matokeo yake? Wakala wa Airtel ndiye aliyebaki amepoteza pesa, huku mdada akirejeshewa hela yake bila matatizo.
Sasa, Airtel Money inawalinda vipi mawakala wao dhidi ya hali kama hii? Inawezekanaje fedha zirudishwe bila hata mawasiliano na wakala aliyetoa huduma?
Je, mawakala ndio waendelee kubeba mzigo wa uzembe wa wateja?
Hii ndio sababu watu wengi wanakimbia mtandao wenu!
Utapeli mwingi wa sasa unahusisha mtandao wa Airtel—ni kweli hamjui kinachoendelea au mnafurahia michezo hii?
Kwa nini malalamiko mengi yanawahusu nyie tu?
Ruksa, wengine wajifunzeMkuu kwa ruhusa yako naona Ni copy andiko lako niipeleke kwenye group la mawakala Facebook
Huenda inapaswa wakala adai kitambulisho japo siku hizi tunafanya business as usualHapa ni analia anatamani afunge tu Ofisi yenyewe
Kabisa!! Sasa badala ya Airtel Money wawe fear, wao wanafanya maamuzi ya upande mmoja!! Haina maana kuwa wakala wa Airtel Money kama wanachukulia mambo rahisi hivi.
Humu jukwaani nyuzi kibao zinalalamikia Airtel Money, lakini wapo kimya!!
Inawezekana vipi laini 2 za namba moja zikawa hewani kwa wakati mmoja. Unapo swap maana yake unaiua mojawapo ya laini!Kuna mdada anayeishi Tabata, ambaye aliwasajiliwa laini na mawakala wa Airtel waliokuwa wakipita mitaani.
Bila yeye kujua, mawakala hao walifanya SIM swap kwenye laini yake. Baadaye, wale waliosajili laini hiyo waliitumia kwenda kwa wakala wa Airtel Money na kutoa pesa kwa njia halali—simu ikiwa na laini sahihi, namba ya siri ikiingizwa, na pesa ikitoka kama kawaida.
Wakala, bila kujua kuwa anahudumia tapeli, alitoa pesa taslimu.
Mdada aliyekuwa mmiliki wa laini hiyo alikuja kugundua kuwa pesa zake zimetolewa alipokea ujumbe wa uthibitisho.
Alipopiga simu Airtel Money, fedha zake zikarudishwa bila hata wakala aliyetoa pesa kuarifiwa. Matokeo yake? Wakala wa Airtel ndiye aliyebaki amepoteza pesa, huku mdada akirejeshewa hela yake bila matatizo.
Sasa, Airtel Money inawalinda vipi mawakala wao dhidi ya hali kama hii? Inawezekanaje fedha zirudishwe bila hata mawasiliano na wakala aliyetoa huduma?
Je, mawakala ndio waendelee kubeba mzigo wa uzembe wa wateja?
Hii ndio sababu watu wengi wanakimbia mtandao wenu!
Utapeli mwingi wa sasa unahusisha mtandao wa Airtel—ni kweli hamjui kinachoendelea au mnafurahia michezo hii?
Kwa nini malalamiko mengi yanawahusu nyie tu?
Kuna wakati umenielewa vizuri na kuna wakati hujanielewa, baadhi ya maelezo yako ni sahihi.kama ni kweli basi airtel money si wakufanya nao kazi..mm nimejiuliza inawezekana vp tapeli aswap line akatoe hela kwa wakala kirahisi tu mfano 50,000 mkononi alafu mwenye laini yake anapiga simu airtel money arudishiwe pesa yake na kweli inarudishwa..swali langu hiyo hela imerudi kutoka wapi ikiwa tapeli alipewa hela mkononi inamaana airtel wanampa pesa ya bure aliyetapeliwa.? au hela wanayorudisha wanachukua kwa wakala hivyo atapoteza pesa mara mbili au.?..swali lingine hao airtel wanadhibitisha vp huyo aliyepiga simu kwao ametapeliwa maana kwa jinsi ulivyoeleza hapa mtoa mada hata ww mwenye laini yako hio unaweza kufanya huo mchezo yaani utatoa hela yako kihalali kwa wakala alafu unasogea mtaa wa pili kisha unawapigia simu airtel money kwamba hela yako imetolewa unaomba warudishe na hao airtel walivyo mapoyoyo wanarudisha kweli hiyo hela je,wao wameitoa wapi hio hela waliyokurudishia ww.? na wakirudisha ww tena unaenda kwa wakala mwingine unatoa tena mara ya pili hivyo unapata double.!kwa maelezo yako mtoa mada mbona kama haiingii akilini urahisi namna hii kwani hata ww mwenye laini yako unaweza kufanya sio lazima tapeli..hii story kuna kitu kimepotoshwa kwa chumvi nyingi vinginevyo haifai kuweka airtel money kwenye biashara ya miamala au ubuni njia zako kuidhibiti hio loophole.
Ndio swali la kujiuliza, aliyetapeliwa alipate sms kuwa laini yake imetolewa hela hadi akaamua kupiga simu kuomba irudishwe.Inawezekana vipi laini 2 za namba moja zikawa hewani kwa wakati mmoja. Unapo swap maana yake unaiua mojawapo ya laini!
Kuna wakati umenielewa vizuri na kuna wakati hujanielewa, baadhi ya maelezo yako ni sahihi.
KI ufupi ni kuwa, aliyetapeliwa kwa uzembe wake, yeye alichofanya ni kupiga simu Airtel akasema muamala urudishwe, ukarudishwa bila yule wakala kupigiwa Simu. Kumbuka wakala alimuhudumia tapeli kama anamuhudumia mteja mwingine, maana alifika akaomba kutoa Airtel Money, akatoa kweli, akapewa Cash yake, Kwa nini Airtel walivyopigiwa simu warudishe wakarudisha tu kirahisi? Ndio msingi wa Swali lao pia, kuwa basi wengi sana watatapeliwa kama simu ikipigwa tu Muamala unarudishwa...mtu atatoa hela mtaa A zen anazunguka Mtaa B anapiga simu kuwa anaomba muamala urudishwe anarudishiwa.
Cha kujiuliza, kwa nini iwe Airtel tuu, angalia hata humu jamvini, wanaolalamika ni kuhusu Airtel tuu, kwa nini iwe kwao tu?
Kabla hujaipeleka unajua kuwa unapotoa pesa kwa wakala sheria inassemajee,? Na hyo vigezo wanazingatiaa? Tafakari kwanza isjekua niyale mambo ya yanga kumpeleka Morson cas (niwawili tuu)Mkuu kwa ruhusa yako naona Ni copy andiko lako niipeleke kwenye group la mawakala Facebook