Mwananchi hewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2016
- 226
- 274
Utapeli wao ni hivi
Mimi niliweka kiasi cha shilingi laki mbili kwa mwezi mmoja katika timiza akiba yao, na wao walisema mteja atakayeweka pesa ndani ya mwezi mmoja bila kutoa basi atapata asilimia tano ya kiasi cha pesa alichoweka ndani ya mwezi huo lakini katika laki mbili niliyoweka nimepewa tsh 73 tu japo sikuweka hela kwa mkupuo.
Kwanini naamini wamenitapeli?
Baada ya kupata kiasi hicho kidogo cha fedha nisichotegemea kwa maana mimi nilitegemea kupata kama elfu kumi hivi, nilienda katika akaunti zao za mitandao ya kijamii sikujibiwa tena swali langu linarukwa wanajibiwa wengine.
Ila kali zaidi ya kuonesha ni matapeli nimepiga simu tofauti tatu kwa siku tofauti huduma kwa wateja kila simu moja ina ufafanuzi tofauti kuhusu mnyambuliko wa kuipata asilimia tano
Ya kwanza
Hii nilijibiwa kuwa hiyo asilimia tano unaipata kidogo kidogo kutokana na ulivyoweka hela katika akaunti yako. Yaani kwa mfano umeweka pesa tarehe 3,5,7,12,27, basi mwezi ujao zikifika hizo tarehe unalipwa hela yako kutokana na tarehe ulizoweka. Mimi nikakubali nikawa nasubiri hela yangu ila ni tofauti mpaka leo kiasi ni kile kile cha mwanzo hakuna kilichozidi, ikabidi nipige simu tena
Ya pili
Hii nikauliza 5% mteja anaipata vipi na nikawaambia kiasi changu nilichoweka, huyu akanijibu hivi
Kiasi nilichoweka ndani ya mwezi mzima kinagawanywa mara 12 halafu hiko kiasi kilichopatikana asilimia tano yake ndio nalipwa, hapa ndipo huu utapeli nikatulia siku kadhaa leo nikapiga tena.
Ya tatu
Simu niliyopiga leo nikajibiwa kuwa kiasi nilichoweka kwa mara ya kwanza 5% yake ndiyo nitakayopewa.
Sasa hapo nikaamini ni utapeli maana simu zote tatu ufafanuzi ni tofauti.
Siyo kwamba naumia ila wamevunja makubaliano waliyosema.
Sent using Jamii Forums mobile app