Airtel mbona mnatupandishia bei ya bundle bila taarifa?

Godwin Mneng'ene

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2010
Posts
215
Reaction score
86
Nimesikitishwa na kitendo cha kampuni ya Airtel kupandisha gharama ya bundle kwa viwango vya kuruka kama ifuatavyo;

Receive:
Chagua Kifurushi cha

1. 25mb (Tsh. 1500)
2. 150mb (Tsh. 6000)
3. 250mb (Tsh. 10000)
4. 500mb (Tsh. 12000)
5. 1gb (Tsh. 15000)
6. 2gb (Tsh.
# Next


kwa bei hii wateja wengi tumeshakimbilia ttcl, embu punguzeni hizo gharama ni kubwa sana kwa sisi wa tz wa kawaida tafadhalini mturudishie bundle 400mb kwa 2500Tsh kwa mwezi. Nategemea mtasikia kilio hiki.

 
Katika watu wajinga ni hao Airtel wameona watanzania wamezoea banadle ya 400mb kwa tshs. 2500 wameamua kutuletea uhuni wao. Ukiweka bandle ya 400MB ukiangalia facebook dk 50 lote limeisha manake nini kama c upuuzi huu. Mods kuweni makini sana tunajua Airtel wana matangazo kwenye web yenu ila tuacheni tuwaeleze ukweli kwani bila internet yao wengine sie tusingekuwa tunaingia humu kwenye JF. Shame on u Airtel for the pooooooooooooooor service to your customers.
 
nadhani wanafanya biashara na mlikibilia huko kwa kuwa mliona na nafuu kuliko kampuni zote.yafaa kanza kuwashukuru kwa kuwasaidia kwa kipindi chote hicho.hiyo ilikuwa ni kama promotion na ililenga sana kwa simu za mkononi na watu wakaipindisha na kudhani itadumu milele.kuna bepari anayetaka kupata hasara?kisha uza modem za kutosha na watu wengi wamehamia huko.ingekuwa hizo bandwith wanatengeneza wenyewe sawa lakini kuna sehemu wanakonunua na wao ili wpate faida lazima wakuonjeshe kapromo kidogo ukinogewa wanakata ili ununue halisia
 
kwani huko ttcl ni rahisi?au wameboresha ile unlimited ya buku kwa saa?
 
Kama umeshindwa gharama, hama mtandao wacha kulalamika. Kuna mtu kakulazimisha?
 
Airtrel jifunzeni kua na ustaharabu, ni vyema mge tutaarifu wateja wenu, then kwa jinsi iyo rate ilivyopanda kwa kiwango kikubwa mngepaswa kutoa sababu za msingi.
 
Acheni kulalamika kama gharama zimewashinda hamieni kwenye urahisi ila ndio mjue vya rahisi gharama vilevile
 

Si kweli. sasa hivi nimenunua bundle ya 400Mb baada ya kusoma post yako.
usipotoshe umma
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…