Airtel mnatapeli wateja wenu wa router

Airtel mnatapeli wateja wenu wa router

Mshamba wa kusini

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2015
Posts
2,857
Reaction score
3,593
Mwezi uliopita nilienda Airtel shop kununua router kwa ajili ya internet. Nilipewa options mbili nipewe router bure na niwe nalipia kifurushi 110,000 kila mwezi au ninunue router 200,000 alafu niwe nalipia kifurushi 70,000 kila mwezi.

Mi nikalipa 200,000 na kifurushi cha 70,000 kwa mwezi wa kwanza. Hii ya mwezi wa kwanza alinilipia wakala wao wa Airtel moja kwa moja. Baada ya kifurushi kuisha mwezi unaofuatia ambao ndio huu kila nikiingia kwenye menu nakuta natakiwa kulipa 110,000.

Nimeangaika sana kuwapigia simu ili wanirekebishie niweze kupata kifurushi cha 70,000 kama tulivyokubaliana lakini danadana ni nyingi. Hivi sasa ni wiki ya pili sina huduma ya internet.

Soma Pia: Huduma ya Airtel kwa Wateja wa 5G ina walakini, iangaliwe

Airtel mnapoteza wateja HUU NI UTAPELI MCHANA KWEUPE.
 
tapeli katapeliwa na wewe watapeli mkutane mahakamani kinguchiro nguchiro
 
Bora wewe, Mimi nilichukua Router ya Tigo. wenyewe wanatoa Router Bure, kifurushi cha chini nikalipia 100,000

Tangu nilipie Haijawahi kufanya kazi kila siku nikawa naenda Tigoshop lakini wapi, nikaona niachane nayo.

Kumbe Deni lilikua linakua bhana, Mwisho wa siku deni limefika 200,000. Na kumbuka nina laini mbili, Laini primary (Ya matumizi ya kila siku) na Line ya kwenye Router.

Wakafunga line yangu ya matumizi ya kila siku, mpaka nilipolipia huduma ambayo siitumii, washenzi sana hawa watu
 
Huyo wakala ndo kakufanyoa uhuni.. Hapo amekupa Router ya Kibiashara ambayo kawaida hutolew bure(Unalipia kifurushi tu cha 110K ) Alafu kila mwezi ndo utakuta wapaswa kulipia sasa hiyo hiyo 110k au juu zaidi..

Ukipewa ile halali ya 70k hamna hayo mambo.
Tatizo wamewapa matapeli wakiwakala hizo kazi nao huangalia njia zao za kupiga hela.

Nilokuwa nayo nililipa 270k kwa wakala muaminifu, haijawahi niletea shida yoyote
 
Waendelee kumuomba Mungu tusipate Rais mwenye akili timamu ambaye ataruhusu Elon Musk kutoa huduma za Internet!

Yaani waombe usiku na mchana lakini vinginevyo muda hauko mbali ambao watalia na kusaga meno!

Ngoja tuupe Muda Muda!
 
Waendelee kumuomba Mungu tusipate Rais mwenye akili timamu ambaye ataruhusu Elon Musk kutoa huduma za Internet!

Yaani waombe usiku na mchana lakini vinginevyo muda hauko mbali ambao watalia na kusaga meno!

Ngoja tuupe Muda Muda!
ipo siku
 
Ivi airtel wana line ya huduma kwa wateja kuongea na mhudumu mojakwa moja?
 
Shida tuu ni ukweli ambao watu hawaambiwi kuhusu hizi huduma za unlimited,
Iko hivi kwenye kila mtandao unaoambiwa unapewa bando unlimited hua kuna "behind".
Hichi ni kiwango cha gb unachopewa nyuma ya pazia yani mfano kwenye hiyo ya artel unakuta wanakupa tb 1.2 so ukitumia ikiisha hata kama umemaliza ndani ya siku tano basi hapo mtandao utashuka speed hadi 2mbps. So kabla huja nunua kifaa cha wifi lazima upate mtu ambae hayupo ki biashara anaeweza kukupa in deep kuhusu aina ya package unayoenda kuchukua kulingana na matumizi yako mana matumiz yanatofautiana na hua mitandao inaweka bei kulingana na thamani ya kitu, na ukipima kitu kulingana na thamani hua ni kama mitandao yote bei zinalingana

Nikikuuliza maswali yangu nikajua unahitajika uwe na router ya aina gani kulingana na matumiz yako hutojutia hela yako uliyotoa kuknunua router

Ushauri ni bure ila itakua vizuri ukinicheki kwa namba yangu cause ku post hapa inaweza kusababisha nionekane naharibu baadhi ya biashara za watu.
Nicheki 0717700921
 
Back
Top Bottom