GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,286
- 6,736
Sikutegemea kwa kampuni kubwa kama Airtel kuwa wazembe na wasumbufu namna hii. Unapopiga simu kutaka kurenew Line unaambiwa nunua Line mpya halafu hakikisha una kitambulisho chako ulichosajilia simu au namba tano za watu uliowapigia mara ya mwisho au kasha la line iliyopotea au kuibiwa. Kama unavyo vitu hivyo piga 0 ili kupata msaada kutoka huduma kwa wateja au nenda kwa mawakala wetu. Ukipiga sasa hiyo sifuri unaambiwa uende tena kwa mawakala hata ukiwaomba vipi hawakubali! Jamani Airtel huu ni usumbufu na kibiashara mmefeli kusatisfy mahitaji ya wateja wenu. Si ustaarabu kwa kampuni kubwa kama hiyo kufanya ujinga huo unaoendelea, Hebu fanyeni mambo kisomi!