Airtel wamezindua 4G internet connection prematurely, bado hawajajipanga

Airtel wamezindua 4G internet connection prematurely, bado hawajajipanga

The Assassin

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
4,942
Reaction score
20,077
Mimi nilianza kutumia mtandao wa airtel baada ya wao kutangaza kuanza mawasiliano ya mfumo wa 4G, nikajua labda wataleta mapinduzi dhidi ya vodacom 4G ambayo nimekua nikitumia kwa miaka zaidi ya 2 iliyopita, ila imekua kinyume na matarajio yangu, 4G ya airtel ni ya hovyo kuliko 3G ya vodacom.

Nadhani airtel hawakua wamejipanga kabla hawajazindua huu mfumo wa mawasiliano wa data wa 4G. Airtel wana vifurushi bomba kabisa ila havina maana kwa sababu hakuna uzuri wake, airtel 4G video clip za whatsapp statuses huwezi kuangalia moja kwa moja, sekunde kadhaa, inastak, sekunde kadhaa inastak. Hua inakua vizuri muda wa usiku tu.

Airtel jipangeni, haya mambo hayahitaji uharaka bali maandalizi. Pamoja na hilo bado nitawapa muda zaidi nikiamini mtabadilika, vinginevyo nyie sio wazazi wangu.
 
Kweli watakuwa hawajajipanga,kwenye Ramani wanaonekana wapo mikoa mingi,ila kiuhalisia hawajafika.
 
Mbona Tigo tunatumia 4G huu mwaka wa nne sasa? Mbona Airtel wamechelewa hivyo?
 
Hawako vizuri kabisa noor soon nitaachana nao.
Kwanza UNI OFA ni meaningless hakuna OFA hapo.
Nikiwa Chuo napata GB 1 kwa wiki nikija Geita hakuna hicho kitu sasa nini maana ya Line za chuo?
Vitambulisho vya chuo walivihitaji vya nini?
Airtel wanakera sana.
 
Back
Top Bottom