Aisee! Kumbe ufugaji wa Mbuni (Ostrich) una faida na utajiri mkubwa?

SUPER PREDATOR

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2014
Posts
2,093
Reaction score
725
Jamani wanajamvi wenzangu,

Katika kupitia makala mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali duniani nimegundua kuwa ufugaji wa mbuni una faida kubwa sana na hauna gharama kubwa kwa sababu mbuni anapendelea kula majani kama chakula chake kikuu, gharama kubwa ambayo muwekezaji anayeanza kuwekeza ataingia ni ardhi kubwa isiyopungua heka mbili na ujenzi wa uzio (fency).

Tatizo kubwa ambalo mimi naliona ni upatikanaji wa vifaranga au mayai ya mbuni kutoka mamlaka ya hifadhi ya wanyama poli Tanzania na idhini ya ufugaji kutoka serikalini au taasisi inayohusiana na mambo hayo (mimi sifahamu taasisi yeyote inayouza vifaranga au mayai ya mbuni).

Naomba wenye kujua namna ya kutatua hilo tatizo nililoliona wanisaidie.

Tafadhali wanajamvi karibuni kwa mjadala.
 
hii ya leo kali lakini ni jambo linalowezekana! ungejaribu kutupa faida na utajiri unaoweza kupatikana kwa kufuga mbuni kwanza then watu watathmini/ thanks
 
Kuna mtu hapa bongo katika mapori ya Lugoba Chalinze anafanya ufugaji wa mbuni na mpaka sasa soko la mayai ya mbuni for export limemshinda yaani soko limekuwa kubwa zaidi ya uzalishaji

hii ni changamoto ..... vibali kwa ajili ya ufugaji vinatolewa na wizara ya maliasili na utalii ikishirikiana na ofisi ya mazingira ... cha ajabu ili mbuni wa kiume aweze kumpanda wa kike anahitaji angalau umbali wa nusu kilometer kwa ajili ya kumkimbiza jike na kumkwea

mayai ya mbuni yanaagulika kirahisi kwenye incubator ... yai moja linafika hata kilo 3 .... mbuni aliyeekomaa anafikia uzito wa mpaka 70kg
 
kuna mtu hapa bongo katika mapori ya Lugoba Chalinze anafanya ufugaji wa mbuni na mpaka sasa soko la mayai ya mbuni for export limemshinda yaani soko limekuwa kubwa zaidi ya uzalishaji

nashukuru kwa mchango wako mkuu.
 
yaani wenzio tupo kwenye kampeni ya kumaliza ujangili we ndio unafikiria kabisa kufuga? kaa chini nasema kaa chini
Dah mkuu mbona comment yako haiendani na jukwaa ulilopo??

Huku tunajadili bussiness ideas na namna ya kujikwamua kiuchumi wewe unaleta mzaha wa jukwaa la siasa mkuu..

Mtoa mada kazungumzia mpaka suala la vibali ya serikali, sasa ujangili unatoka wapi hapo??
 
kuna mtu hapa bongo katika mapori ya Lugoba Chalinze anafanya ufugaji wa mbuni na mpaka sasa soko la mayai ya mbuni for export limemshinda yaani soko limekuwa kubwa zaidi ya uzalishaji

hii ni changamoto ..... vibali kwa ajili ya ufugaji vinatolewa na wizara ya maliasili na utalii ikishirikiana na ofisi ya mazingira ... cha ajabu ili mbuni wa kiume aweze kumpanda wa kike anahitaji angalau umbali wa nusu kilometer kwa ajili ya kumkimbiza jike na kumkwea

mayai ya mbuni yanaagulika kirahisi kwenye incubator ... yai moja linafika hata kilo 3 .... mbuni aliyeekomaa anafikia uzito wa mpaka 70kg

Mkuu umeongea pwenti kubwa mbili hapa za msingi sana, naomba ufafanuzi zaidi

1)Vibali kumbe vipo na watu binafsi wanaruhusiwa kufuga mbuni bila bugudha yoyote toka kwa watu wa maliasili??

2)Hio nusu kilometa ambayo mbuni dume anahitaji kumfukuza mbuni jike inatakiwa kuwa ni umbali ulionyooka au hata kama una hekari kumi mathalani na mbuni wakafukuzana humo humo kwa kuzunguka zunguka bado inafaa??
 
haya nimawazo mazuri..mwenye uelewa nayo atutiririshie mahitaji muhimu yambuni ili aishi bila matatizo,.nagharama kwa ufupi..
 
Ni wazo zuri tunaomba wadau watusaidie mawazo ya namna ya kuanza hasa kwa mtu alie na ardhi tayari
 
Mkuu umeongea pwenti kubwa mbili hapa za msingi sana, naomba ufafanuzi zaidi

1)Vibali kumbe vipo na watu binafsi wanaruhusiwa kufuga mbuni bila bugudha yoyote toka kwa watu wa maliasili??

2)Hio nusu kilometa ambayo mbuni dume anahitaji kumfukuza mbuni jike inatakiwa kuwa ni umbali ulionyooka au hata kama una hekari kumi mathalani na mbuni wakafukuzana humo humo kwa kuzunguka zunguka bado inafaa??

mkuu .... ukifuatilia vibali utapata bila tatizo .... ingawa urasimu (bureaucracy) wa procedures na rushwa ni changamoto

kuhusu huu umbali .... haya ni makisio yaliyofanywa kwa utafiti wa kimazingira ya mbuni ... umbali huu ni distance ambayo siyo yenye specific direction it is not vector .... hivyo sio umbali myoofu

ufugaji wa mbuni unaokubali vizuri ni free range hapa utaona wafugaji wengi huwa na eneo zaidi ya hekari 20

mambo yapo mengi yanayohusu maendeleo ya kiuchumi ..... kwa wenye mitaji mikubwa kama europe na kwingine ni rahisi sana kufanikiwa kwa mtu mmoja mmoja ... lakini ninaamini kwa nchi masikini na zinazoendelea kama Tanzania tunahitaji umoja na kuunganisha guvu za mawazo, rasilimali watu na mitaji fedha ili kuweza kusonga mbele ... ninashauri watu waungane kufanya miradi kama hii ya ufugaji wa mbuni ambayo pia inahitaji muda mwingi wa utafiti na uwekezaji kitaalamu
 
Shurani sana mkuu, angalau hapo kwenye suala la umbali umenipunguzia tension yangu.

Nafikiri kwa suala la kufuga kwa mtindo wa free range kuna mambo ya msingi ambayo inatakiwa yazingatiwe na ndio maana maswali makubwa yaanza kuibuka hapa

1)Stocking density kwa eneo ikoje?? say hekari kama ishirini mtu unaweza kufuga mbuni wangapi??

2)Kama unamua kuwa unawapa chakula cha ziada maana najua hawawezi kutegemea chakula cha kujiokotea kila siku , ni chakula gani wanakula??

3)Mbuni ata vitabia tofauti na ndege wengine, je analala na kutaga kwenye mabanda au kwenye vichaka??
 
mkuu .... no. 1& 2 unaweza ku-google ukapata jibu

kuhusu point number 3 .... wanyama wengi hasa hawsa jamii ya ndege (Aves) origin yao ni porini lakini kutokana na habitat na ecology basi binadamu wanatengeneza mazingira mapya ya maisha kwa hawa viumbe ili waweze kuwacontrol kwa manufaa ya maisha ya binadamu (economic purpose) hivvyo basi kwa kutumia taaluma mbali mbali za biolojia na sayansi mbuni hawa wamaanguliwa artificially na kuwa hawana mama hivyo huanza kuishi katika mazingira tofauti na porini wakifuata matunzo yenye matakwa na hitaji la binadamu .... hii hupelekea wao kubadili baadhi ya tabia za kuishi na ku-adapt maisha na mazingira ya kufugika

mbuni pia hutoka nje asubuhi na jioni kuingia kwenye banda ..... mbuni hutengenezewa sehemu ya kutagia mithili ya kichaka mbali na anapolala
 
sasaa kama inahitajika nusu kilomita ili jamaa apewe mzigo ukiwa na mbuni 50 mbona itakua kazi sana!
Ngoja nami nifwatilie.

Mkuu umenikumbusha Mtakuja Primary School,yai moja linaiva kwa dakika tano,je,mayai matano yataiva kwa dakika ngapi?Unamaanisha ukiwa na mbuni wanne,majike mawili na madume mawili inaitajika uwe na kilometa moja!
 
Sio mbuni tu hata tausi.
Kenya Tausi 1 wa miezi 4 mpaka 6 anauz2a laki 7 ya bongo..mkubwa mpaka 1m.Tz tunakosa fursaa
 
Back
Top Bottom