Aisha Madinda: Jinsi madawa ya kulevya (unga) yalivyonifilisi

kipenga

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
219
Reaction score
55
WIMBI la uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya limeshika kasi hivi sasa kwa wasanii na watu mbalimbali huku Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe akilivalia njuga kulikomesha.

Wakati hayo yakiendelea, mnenguaji aliyetikisa anga la muziki wa dansi nchini, Aisha Mohammed Mbegu ‘Aisha Madinda’ amejuta kutokana na kufilisika baada ya kutumia madawa ya kulevya.

Akizungumza katika mahojiano maalum na gazeti la Ijumaa hivi karibuni, Aisha alisema alipokuwa juu kwa unenguaji alifanikiwa kumiliki mali mbalimbali zikiwemo nyumba tatu pamoja na gari lakini madawa yamemlostisha.

Akisimulia jinsi nyumba zake tatu zilivyopotea, Aisha alisema alianza kuweka rehani ‘bondi’ nyumba yake ya Kigamboni akiwa anachukua fedha kidogokidogo hadi alipoambiwa fedha zake zimekwisha.

“Baada ya kuiweka bondi nyumba ya Kigamboni na kuambiwa sina changu nikaenda kuuza nyumba ya Kimara mwisho,” alisema.

Baada ya kumaliza nyumba zake, mnenguaji huyo akadai kuwa aligeukia gari lake aina ya Toyota Mark II ambalo nalo aliliuza.

“Niliona ujinga nilikuwa nikipata tabu ya kutafuta fedha za kununulia unga wakati gari nilikuwa nalo, nikaisukumia mbali,” aliongeza huku akisikitika kwa uamuzi huo ambao sasa anaujutia.

Aidha, Aisha alisema hivi sasa anawachukia wanaouza madawa ya kulevya kwa kuwa wanatajirika wakati wao kama watumiaji wanafilisika kifedha na kuumia kiafya.

“Sisi wanunuzi tunakuwa na maisha magumu wakati wenzetu wanatajirika,
binafsi sikuwahi kutegemea kama ningeishi maisha kama haya, nawashauri mastaa wengine wanaondelea kutumia madawa hayo waache mara moja kwani madhara yake ni makubwa kiuchumi na kiafya,” alimalizia mnenguaji huyo ambaye hivi sasa yuko fiti na anaweza kupanda jukwaani wakati wowote.
 
Nilikuwa natamani nijaribu siku moja ili nijue hizo stimu zinakuwaje ila kwa ushauri huu nimekoma

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Nilikuwa natamani nijaribu siku moja ili nijue hizo stimu zinakuwaje ila kwa ushauri huu nimekoma

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums

yaani usijaribu hata kwa bahati mbaya
 
Huyu dada alikuwa mzuri sana,, lkn sasa kapotea hawezi hata kujipanga tena,pole Aisha.
 
Stimu utakayopata siku ya kwanza inashawishi urudie tena na tena
 
Nilikuwa natamani nijaribu siku moja ili nijue hizo stimu zinakuwaje ila kwa ushauri huu nimekoma

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums

Umeona eeeeeeeeeeehhhhhhhh! Kama jina lako lilivyo Usiniguse, basi husiguse.
 
...duuh! nilikuwa sijajua kama huyu dada nae alikuwemo, kumbe tatizo ni kubwa kuliko hata wengine tulivyokuwa tunafikiria....
 
Nilikuwa natamani nijaribu siku moja ili nijue hizo stimu zinakuwaje ila kwa ushauri huu nimekoma

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums

dont dare,wenyewe wanateseka sana aisee,nimefanya kazi na moja ya NGO

inashughulika na mambo ya drugs wao wenyewe wanalia bana
 
...duuh! nilikuwa sijajua kama huyu dada nae alikuwemo, kumbe tatizo ni kubwa kuliko hata wengine tulivyokuwa tunafikiria....

upo kijiji gani kwani?ktk mateja maarufu kinondoni Aisha ana namba yake,yeye mwenyewe alianzisha biashara yake akampa mtu auze matokeo yake aliishia kujikopesha mwenyewe na muuzaji wake akawa teja pia biashara ikafa,
alikuwa akija msisiri anaomba afungiwe mlango na kufuri kwa nje,anavuta dona mpaka anazima wahuni wanafungua mlango wanapiga mashine watakavyo wanamwacha hoi wanasepa!siku ambayo hapigwi mashine labda kaja na banza au diof wawe wanavuta wote!
Mi nina wasiwasi kama hana HIV tu!
Ray c ndo alikuwa anakuja na lord eyez wanapaki prado yao pembeni wanavuta wanasepa nae alikuwa akija peke yake watu wanapiga mashine akizidiwa yani hao UKIMWI nje nje..
 
duuh! nilikuwa sijajua kama huyu dada nae alikuwemo, kumbe tatizo ni kubwa kuliko hata wengine tulivyokuwa tunafikiria....[/QUOTE]

upo kijiji gani kwani?ktk mateja maarufu kinondoni Aisha ana namba yake,yeye mwenyewe alianzisha biashara yake akampa mtu auze matokeo yake aliishia kujikopesha mwenyewe na muuzaji wake akawa teja pia biashara ikafa,
alikuwa akija msisiri anaomba afungiwe mlango na kufuri kwa nje,anavuta dona mpaka anazima wahuni wanafungua mlango wanapiga mashine watakavyo wanamwacha hoi wanasepa!siku ambayo hapigwi mashine labda kaja na banza au diof wawe wanavuta wote!
Mi nina wasiwasi kama hana HIV tu!
Ray c ndo alikuwa anakuja na lord eyez wanapaki prado yao pembeni wanavuta wanasepa nae alikuwa akija peke yake watu wanapiga mashine akizidiwa yani hao UKIMWI nje nje..
 
...duuh! nilikuwa sijajua kama huyu dada nae alikuwemo, kumbe tatizo ni kubwa kuliko hata wengine tulivyokuwa tunafikiria....

hii issue ni kubwa sana, ila watu wengi wanafungua sana tofauti na miaka ya nyuma, nadhani matumizi yake yatapungua pia
 
kama aisha madinda amefirisika basi mimi ni billionea maana nilikuwa sijui tafsiri ya tajiri bongo
 
Asha baraka mwenyewe teja anatumia methadone
 
senbe noma,mi namsikitikia daz baba jamani, dah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…