Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Aishangaza Mahakama
Advertisement
Saturday, April 18, 2009 9:57 AM
MSHITAKIWA huyo anayekabiliwa na kesi ya kosa la kuuza dawa za kulevya aina ya bangi ametoa kioja mbele ya Mahakama kwa kutambua kuwa anachokisema si kosa.
Mshitakiwa huyo ni Kalinga Kibadeni mkazi wa jiji la Dar es Salaam alifikishwa Mahakamani kwa kosa la kuuza bangi.
Mshitakiwa huyo aliishangaza Mahakama wakati alipokuwa anatoa utetezi wa kesi yake hiyo inayomkabili na alipotakiwa kujitetea ili asiweze kupata adhabu kali.
Mshitakiwa huyo alidai kuwa na kutoa msisitizo mbele ya Hakimu Samweli Maweda kuwa yeye amebambikiziwa kesi hiyu kwa kuwa yeye hauzi bangi ila yeye anavuta bangi.
Mwendesha Mashitaka wa kesi hiyo Naima Mwanga alimwambia tena ajitetee ili asiweze kupewa adhabu nzito kwa kuwa ushahidi na vielelezi vilishakamilika na kupatikana na hatia.
Mshitakiwa huyo alirudia tena kwa kusema kuwa anaomba asipewe adhabu kwa kuwa yeye sio muuzaji wa bangi ila ni mvutaji mzuri wa bangi.
Mheshimiwa mimi ni mvutaji mzuri sana wa bangi na siuzi bangi mheshimiwa hakimu alijitetea mshitakiwa huyo
Aliendelea kwa kujitetea kuwa anaomba asipewe adhabu kwa kuwa kesi iliyomfikisha Mahakamani hapo amebambikiziwa na si kweli ila bangi anakubali anavuta.
Alisema mimi navuta bangi kulingana na kazi zangu ngumu ninazozifanya za kubeba mizigo sokoni Kariakoo ndio mana navuta bangi iweze kunisaidia
Awali mshitakiwa huyo alifikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa kosa la kuuza bangi.
Ilidaiwa kuwa Julai 14, mwaka juzi, mshitakiwa huyo alikamatwa na askari akiwa na misokoto 76 ya bangi katika soko la Kariakoo
Kwa kuwa ushahidi umeshafungwa na mshitakiwa amekwisha toa utetezi Hakimu aliahirisha kesi hiyo hadi Aprili 30, mwaka huu, itakapokuja kwa hukumu.