Kwa mujibu wa mtandao wa michezo wa Sofascore, golikipa mahiri wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Simba, Aishi Manula, hadi sasa ndiye mwenye rating kubwa kuliko magolikipa wote walio na timu zinazoshiriki michuano ya CHAN huko Cameroon. Hii ni hadi round ya tatu inapokamilika hapo jana.
Hata AFCON mechi mbili za makundi alikuwa na saves nyingi kuliko. Tafsiri ya saves nyingi huenda ikawa ubora wa golikipa au udhaifu wa safu ya ulinzi kuruhusu lango lao kusogelewa maradufu au yote kwa pamoja.