Aishi Manula: Sijasajili Simba

Aishi Manula: Sijasajili Simba

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Mlinda mlango wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Aishi Salum Manula, amekanusha kusaini na Klabu ya Simba huku akiongeza kuwa vipo vilabu vingi vya hapa nchini alivyofanya navyo mazungumzo na muda ukifika itajulikana na timu gani ataitumikia.

[Hébergement Internet, Cloud, et Serveurs dédiés - OVH]

Mlinda mlango wa Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Aishi Salum Manula.

Aishi amekiri kuwa sasa yeye bado ni mlinda mlango wa Azam FC lakini ameshafanya nao mazungumzo na wamekubaliana kuondoka mkataba wake utakapoisha huku akiongeza ya kuwa amepata ofa nyingi za vilabu vya ndani lakini kwa sasa bado sio muda mwafaka wa kutaja klabu atakayojiunga nayo baada ya kumalizana na Azam FC.

“Cha kusema kuhusiana na suala la mimi kutoka Azam FC ilo niwahakikishie mashabiki na wapenda Soka Watanzania kwamba ni kweli mkataba wangu utakapoisha Azam FC nitaondoka ndani ya Azam lakini kuhusiana na ofa ni kweli kuna ofa nyingi nimepata ndani ya nchi na tuliweza kuzungumza na hizo klabu ambazo zinanihitaji na mazungumzo yameenda vizuri na yanaendelea vizuri kwa ujumla” amesema Aishi Manula.

Aishi amekanusha yeye kusaini mkataba na klabu ya Simba

“Mimi sijasaini Simba na nasikia kuna mkataba unaonyesha kwamba nimesaini Simba, hizo nadhani ni watu wanajitahidi kutaka kujua au kuwathibitishia mashabiki waamini kwamba nimesaini Simba lakini sio kweli, na kama ningekuwa nimesaini Simba nadhani wao wenyewe wangeshanitangaza, ” amesema Aishi Manula.

Aishi amesisitiza kuwa mpaka sasa bado hajajiunga na klabu yoyote hapa nchini huku akiwataka mashabiki kuwa tayari kwani muda utakapofika ataweka wazi kila kitu.

“Kuhusiana na kujiunga na klabu yoyote hapa nchini bado na sio muda mwafaka wa mimi kutaja Klabu ambayo nitaenda kujiunga nayo lakini wakae tayari wakinisubiri mkataba wangu utakapoisha Julai mwaka huu ndani ya Azam FC nitaweka wazi wapi naenda lakini kuhusiana na mkataba sio kweli na sijasaini na timu yoyote” amesema Aishi Manula.
 
Hahahaha ! Uyanga wako utakuua bure, mchezaji mzuri km huyo akose timu hadi sasa wakt amesema hataongeza mkataba AZAM,Wewe nawe tikiti maji kweli.
Huyo anazuga tu alishamwaga wino Msimbazi
 
Hata kama hakusaini lakini msimu ujao Manura atachezea Simba! Ni bora akawa wazi tu.
 
Dah, hii timu yetu mbona imekaa ki-iptl iptl?? Walisema wamemsajili Manura, mara Niyonzima kumbe wote hawa chenga hakuna hata mmoja ambaye ameshuka msimbazi. Aden Rage hakukosea kutuita mbumbumbu fc maana viongozi wetu wanatudanganya tu wanavyojisikia. Naanza kuona mapema jinsi tutakavyomiss ubingwa msimu ujao.
 
Tumia akili japo kidogo, hawezi kusema ameshasaini wakati bado mkataba wake haujaisha pale Azam fc
 
Hahahaha ! Uyanga wako utakuua bure, mchezaji mzuri km huyo akose timu hadi sasa wakt amesema hataongeza mkataba AZAM,Wewe nawe tikiti maji kweli.
Huyo anazuga tu alishamwaga wino Msimbazi
Sijui tikiti ni nani hapa. Awe amesaini harafu aseme hajasaini ili iweje?
Kunaweza kuwa na makubaliano ya awali lakini kusaini bado
Sasa ameona fedha inayotajwa kwa Niyonzima na Ngoma. Lazima atingishe pesa iongezeke. Simple and clear!
 
Dah, hii timu yetu mbona imekaa ki-iptl iptl?? Walisema wamemsajili Manura, mara Niyonzima kumbe wote hawa chenga hakuna hata mmoja ambaye ameshuka msimbazi. Aden Rage hakukosea kutuita mbumbumbu fc maana viongozi wetu wanatudanganya tu wanavyojisikia. Naanza kuona mapema jinsi tutakavyomiss ubingwa msimu ujao.
mkuu hawa watu wana mikataba bado na timu zao. hawawezi kusaign sasa ni makubaliano tu yamefanyika no signing mpaka mikataba ifike tamati possibly July.
 
Uyo amesaini tayari ila anahofia sababu bado ana mkataba na Azam kwahyo anasubiri siku ziishe tu
 
IMG-20170627-WA0000.jpg
juma_simba_dihile-20170626-0001.jpg
 
Back
Top Bottom