Kama mtoto ana mwaka na miezi 7 na bahati mbaya ni muathirika, nashauri.
1; Tatizo limeingia kwenye ndoa hakuna haja ya kutafuta mchawi, wanandoa wakae chini wakubaliane na jinsi ya kuishi kwa pamoja na kulea familia yao.
2; Waende kwenye kitengo cha wanaoishi na vvu kwenye hospitali zote za serikali hicho kitengo kipo, waende wote watatu, watapewa ushauri na kupimwa tena kwa umakini wote watatu, baba mama na mtoto.
3; Endapo majibu yatakuwa kama awali baba hana, basi watashauriwa jinsi ya kuishi maisha ya ndoa bila kuambukizana, ambapo baba atatakiwa kutumia kondom sahihi muda wote atakapojamiiana na mkewe na mke asichepuke kupunguza uwezekano wa kupata maambukizi mapya pamoja na magonjwa mengine ya ngono.
4: Waathirika wataanzishiwa dozi mara moja.
Ni muhimu waende wote ili mtu wa afya awachunguze kwa makini,nasema hivo kwa sababi kipimo( sd bioline au unigold) majibu yake lazima usome ndani ya dakika 10 na zisizidi dakika 20, na kuna wakati mwingine mstari mwekundu unaonekana kwa mbali(very weak)
Kwa serikali; nashauri hii iwe funzo, mpango wa serikali kuthibiti maambukizi ya mama kwa mtoto(pmtct) usiishie pale mama anapojifungua, mama aliyezaa bila maambukizi bado afuatiliwe mpaka atakapoacha kumnyonyesha maziwa mtoto, Naswma haya kwa kuchukulia ya kuwa mama aliambukizwa alipoongezewa damu au mama alipata maambukizi baada ya kuujifungua.
Inasikitisha kwa kweli mtoto mdogo kama huyo kuanza kutumia arv, sababu ya uzembe wa madaktari au mfumo kuwa na mapungufu.
Kwa wakunga/watoa afya; Ni uzembe au uuaji kukubali kumzalisha mama bila kujua hali yake ya kiafya, kuna uwezekano mama alikuwa muathirika wakati wa kujifungua na si kwa sababu ya kuongezewa damu.
Kwa wamama wajawazito; epukeni kuongezewa damu wakati wa kujifungua kiuzembe, hakikisha una damu ya kutosha kabla hujajifungua,kula mboga za majani hasa matembele hata kama hayana latha
Poleni sana wanafamilia husika