Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Nipo Mascut nchini Oman. Nimeingia kwenye chumba cha mahakama asubuhi hii kusikiliza kesi ya mmoja wa wanafamilia. Kabla kesi yetu kutajwa nikasikia kesi mchanganyiko.
Iliyonivutia ni hii ya jamaa aliyeamua kupambana na hospitali ya serikali na daktari waliomtangazia kuambukizwa corona na kumpa dawa na kumuweka karantini ya wiki 2 na ilhali hana shida hiyo.
Tulipotoka nje ya mahakama ndipo akatusimulia mkasa wake. Anasema alijihisi na homa na uchofu ulioambatana na kutoka makamasi, akaamua kwenda hospitali.
Alipofika haraka akachukuliwa vipimo na majibu yakaja ana corona. Akapewa dawa za kutumia na masharit akajifungie ndani bila kuonana na watu kwa wiki mbili zinazofuatia.
Kwa vile hakuhisi kitu kigeni sana mbali na mafua anayopata baadhi ya siku hakuridhika na matokeo yale na akaamua kwenda kuchukua vipimo kwenye hospitali nyengine binafsi zilizoruhusiwa kupima corona.
Matokeo kwenye hospitali tatu yakaonesha hana corona na hata mafua nayo si makali sana. Ndipo alipoamua kufungua kesi.