Aitelekeza familia yake kwa penzi la Kitanga!

Aitelekeza familia yake kwa penzi la Kitanga!

Boflo

JF-Expert Member
Joined
Jan 20, 2010
Posts
4,383
Reaction score
4,412
Akimbia familia yake kwa kutekwa na binti wa kitanga
4487422.jpg

Monday, May 17, 2010 10:59 AM
MWANAUME mmoja [40] [jina kapuni] mkazi wa Mabibo Jeshini ,amekiri kuwa amefanyiwa mambo anayohisi ni ya kumpumbaza akili na kujikuta akikimbia familia yake na kuhamia kwa msichana mwenye asili ya kitanga bila kujitambua. Akiongea na mwandishi wa habari hii kwenye mazungumzo ya urafiki, amekiri kuwa inawezekana amefanyiwa kitu mbaya na msichana ambaye hakumtaja jina na kumsahau mke wake na watoto na kwenda kuhamia kwa dada huyo.

Alidai kuwa alipoanza urafiki na dada huyo miezi minane nyuma alikuwa yupo katika hali ya kawaida, lakini ipipotimia kiezi mitano ya urafiki wao alijikuta akiingia katika penzi zito na dada huyo hali ambayo ilimfanya aanze kusahau kidogokidogo familia yake bila kujitambua.

Alidai kuwa alikuwa akienda kwa dada huyo na kuchelewa kurudi nyumbani kwake, mara alijikuta akishindwa kurudi kabisa nyumbani kwake na kulala hukohuko na kumpigia mke wake simu kuwa alikuwa yuko bize kazini na kurudi kesho yake.

Alisema mbaya zaidi alijiona kama yuko tofauti na kuanza kumuona mke wake kama mtu wa kawaida na kumuona dada huyo kama ni mke wake na kuona kamda kitu cha kawaida.

Kutokana na hali hiyo ya kuzidi kusahau familia yake alidai mke wake alikwenda kuripoti kwa ndugu zake yeye na kuulizwa na kukana kuwa si kweli.

Hivyo kadri siku zilivyozidi kwenda hali ndiyo ilizidi kuongezeka ya kusahau familia yake na mke wake kuwataka baadhi ya ya shemeji zake wafike nyumbani kwake walale ili wathibitishe maneno ambayo alikuwa akiwaambia ya kuwa mume wake alikuwa harudi nyumbani.

Shemeji zake hao walithibitisha tukio hilo na kuanza kulifanyia kazi susala hilo na kumfatilia ndugu yao huyo na kugundua kuwa alikuwa akizuzuliwa na mwanamke huyo.

KWa kuwa alikuwa hajitambui ilibidi ndugu hao wamkanye na kumtaka aachane na mwanamke huyo nay eye kukiri ni kweli alikuwa na mahusiano na huyo dada na kuwambia alikuwa anatamani aondokane na hali hiyo lakini alikuwa anashindwa kujinasua kuachana na huyo dada.

“yaani rafiki yangu inawezekana nimeshalishwa limbwata na yule dada kama watu wanavyosema, yaani nimefikia hatua sirudi nyumbani kwangu hii kali? Alisema kaka huyo kwenye mazungumzo na mwandishi wa habari hii

“Na sitamani kumuacha, nimewaambia ndugu zangu mwenye kujua dawa ya kunifanya nirudi nyumbani kwangu anitafutie anipe ili nisisahau kurudi nyumbani kwangu nikienda kwa yule dada, nampenda mkewangu ila ndio hali imenikuta hii” alidai
 
huyo jamaa mzushi tu kama kweli ameshtuka na anakiri anampenda mkewe kwa nn hayo maneno asiende kumwambia mkewe ili akalianzishe kwa hiyo nyumba ndogo? story zingine sijui walisimuliana bar?
 
ni soo ila wakitanga akikuotea fresh mwanangu ubanduki!! utakuwa unamkosa manytimes
 
Wanawake wa kitanga ooooooohh!wanajua kujipamba ooooooooohhhh!hatariiiiiiii. Jamaa inamaana hakujua hayo kabla na uzee wote huo. Kule ndio tanga kutangatanga. Wangoni, warundi,wamakonde,wamanyema,wanyamwezi,wasukuma wengi wao walikwama hasa Pangani. Hii yote ni kutokana na ukarimu wa wanawake na mapishi ya kitanga kama mkate wa mchele, wali wa nazi nk. Pia ukumbuke ukiingia na kutoka mkoa wa Tanga kuna vibao vya karibu Tanga hakuna kwaheri. Mkwakwani, Mapana, Ngamiani mpoooooooooooooooooooooooooooo
 
Hana lolote huyo kajilisha limbwata mwenyewe, kama ameshashtukia bado anafanya nini sasa kwa huyo mwanamke?
 
simshangai kama mambo yenyewe ndo hayo ya Tanga
 
Back
Top Bottom