Ajabu na Kweli ya Zantel!

Mpeni sifa Yesu

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2010
Posts
646
Reaction score
129
Nimejipinda kwa nguvu zangu zote, nikanunua moderm ya zantel ili inisaidia research yangu, nimeenda nayo kimara ninako kaa, nikakuta haifanyi kazi. network yao haifanyi kazi kimara na sehemu zingine za mbezi luis etc. nimejiuliza sana, ni mtandao wa aina gani huu wanaoutangaza sana kuwa internet yao kiboko....unaponunua wanakwambia sehemu zote za dar zinakamata internet. na moderm zao ni mbaya kwasababu ziko fixed, hazitumii sim card kwamba unaweza kubadilisha uweke simcard ya zain au voda kuwakimbia, wanauza garama, kwakweli hapa nimeona kama wameniibia.

kwa wale waliozoea moderm zingine, hasa ulaya, zinakuwa zinatumia simcard, na zingine hata kama ni fixed kwa mtandao mmoja, zinatumia simcard, na ninafikiri unaweza kublock kama unavyoblock simu za mkononi za promosheni vile...hawa jamaa na moderm yao ile ya kukunja, ukinunua ndo umeshanunua...matangazo yao yanatuingiza mjini bwana, badala ya kuwa na net home, sasa mtu hadi nasafiri kwenda kufanyia research yangu maeneo kuanzia ubungo ndo inakamata, badala ya kukaa kwenye kochi langu na kahawa nikawa nafanya mambo kwenye labpot yangu...KAMA KUNA MTU ANAYEHUSIKA HAPA ZANTEL, NAOMBA AREKEBISHE HARAKA, AU MTUJENGEE MNARA NA SISI TUNAOKAA HUKU KIMARA, la sivyo, tutakuwa tumewaungusha tu moderm, hatutanunua credit zenu kabisa. Mungu awasaidie.
 


Please PM me your email address, i will be very happy to assist you.
 
Please PM me your email address, i will be very happy to assist you.

nashukuru, lakini kama unataka kunisaidia, naomba uandike tu hapa ili na wengine wasome wapate faida. ukiniandikia mimi private, haina maana kwasababu ninao uwezo kwenda kununua voda na zain vilevile au ttcl. matangazo yenu tu ndo yalinipiga changa la macho. asante kwa msaada wako. sitakupa email address.
 

Watu wanataka kula commission wewe unataka mambo hadharani huyui hapa kuna PCCB?
 
Watu wanataka kula commission wewe unataka mambo hadharani huyui hapa kuna PCCB?

MI Nilifikiri tatizo ni network, kumbe kuna namna nyingine ya watu kutopata huduma kamili hadi wapitie kwa wataka commission...hahaha. moderm yao wanauza laki moja, nilipie tena kwa mwezi alfu thelathini, alafu hakipatikani kitu, kwanini wanatangaza matangazo matamu sana wakati mtandao wao upo katikati ya jiji tu? sasa sisi wa kimara ndo watu wa mkoa mwingine au vipi?
 


Pole sana ndugu yangu, mimi pia nakaa maeneo hayo lakini kwa kujua uongo huu wa hizi kampuni kabla ya kununua niliomba kwa rafiki zangu na kwenda kutest, mwisho wa siku nilijichukulia tu modem ya kampuni moja ambayo ilifaa, inaonekana kuna sehemu na sehemu hapa Dar ambapo signal zinakuwa strong.
 
mkuu, ungejua, ungeenda Zain au hata TTCL tu. hao zantel bado wanajifunza kazi. wanajifunzia kunyoa kwenye vichwa vya watu wenye akili, badala ya kujifunzia kwenye vicha vya wenda wazimu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…