Ajabu wanaoumia Hersi Said kuwa Rais wa Yanga ni Simba

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Yes twende na Caamil/Hersi Said huyu jamaa typical ni MwanaYanga kindakindaki uzuri wa jamaa hana longolongo akisema amesema inaonekana mwamba hana tamaa ya fedha kama wale wengine jamaa ana malengo ya mbali sana na Yanga hii.

Binafsi naona hata Urais haumtoshi wanayanga tulitakiwa tumpe zawad kubwa zaidi Injinia Sio mchezo kwa akili za juu juu unaweza dhani jamaa katumia akili ndogo kuitoa Yanga ilipo mpaka sasa ila wenye kuufahamu mpira jamaa katumia energy, knowledge, skills, kujitoa, Ibada, fedha, ..nk mpaka kuifikisha Yanga hapa ilipo.

Watu wanaimani na Yanga sasa, makampuni wana imani kubwa sana na Yanga sasa, kila MTU anajua akiweka fedha zake pale Yanga zitakua salama chini ya Mikono ya Hersi Said Injinia.

Huyu jamaa niwa kipekee sana anaipenda Yanga naweza sema ni Yanga Lialia.

Angalia pale Man utd Since ameondoka Ferguson pale ni tia maji tia maji tu ila kwa Kipindi kifupi since Gsm Katia Mikono Yanga chini ya Kijana Injinia Hersi Said tunachukua Vikombe Vitatu tena kutoka kwa timu iliyokua imejipanga kwa fitna zote nje na ndani za uwanja Simba

Tukiacha Ushabiki na chuki cha Kibongo Injinia ni Multi Talented leader Mungu azidi kumlinda na kumjalia hekima zaidi

Kwa mapenzi yake kwa Yanga nachelea kusema ndiye aliyemshawishi GSm kuwekeza pale Yanga.

Wanayanga tungeendelea na kampeni yetu ile ya Bakuli akii leo tungekua tunacheza play off na Prison kupambania kurudi ligi kuu ligi imekua ngumu timu kila siku zinajipanga, Mpira wa kisasa unahitaji Pesa

Kuonyesha Mzee Wetu Msolla anaimani na Kijana wake Injinia Hersi Said kampa baraka zote na kutochukua fomu ya Urais.

Leo jezi za Yanga zinavaliwa kila Kona watu wanaona fahari, Sio mkubwa wala Mdogo,sio baba wala mama leo wanavaa jezi maridadi ya Yanga Ambayo HERSI SAID KAIVUJIA JASHO LA DAMU kapita kwenye milima na Mabonde.

Ndio maana Upande wa Pili Simba wanakuja na Propaganda Uchwara kwa Hersi Said wanajua Urais wa Hersi Said na timu yake ya uongozi Yanga itaenda level za mbali sana I predict siku moja Pitso Mosimane atasimama kwenye benchi la Yanga kama Kocha muda ni Rafiki mzuri.

Simba nyie tulieni tu Hersi Said ndio Rais wa Yanga hata akitaka kuongoza milele tutampa timu, tumejifunza baada ya figisu kwa Manji.

Ndio Huyo Huyo Injinia Hersi Said.
 
Achana nao hao blaza wanataka kupitisha mamluki wao Yanga no door for that wamechelewa hii Yanga ya sasa ukisimama nchale ukikaaa nchale kila idara imejipanga ukija kifigisu tutakujibu kifigisu
#Ndio huyo huyo Injinia Hersi Said.
 
Hersi akili kubwa yule
Kati ya Hazina tulizo nazo Watanzania Hersi ni Kiongozi na sio mtawala popote anafit.

Kaitoa Yanga Mbali sana sishangai watu kumtaja GSm Kila Kona kuna mwandishi mmoja wa kibongo anahoji kwann kombe liende Gsm nlimsamehe tu.
 
Mnawaumiza watu mjue!!!! Siyo kwa sifa hizo.
 
Hersi awe mume wa utopolo wote Ndio cheo kinamfaa.
 
Makolowizard Wana wivu wa kike. Sisi tumeamua Eng Hersi Said ndiyo Rais wa Young African Sport Club na Ni suala muda kila pumzi itaisifia Young Africa kwa mambo makubwa yajayo siku za usoni.
 
Tulia dawa ikuingie, hata waliokuwa wanaumia MO kuwa CEO wa Simba ni Yanga
 
Tulia dawa ikuingie, hata waliokuwa wanaumia MO kuwa CEO wa Simba ni Yanga
Ndio Huyo huyo #Injinia Hersi Said jamaa kawapigeni na chuma kizito sana kichwani kama lile goli la Fei toto
 
Hersi awe mume wa utopolo wote Ndio cheo kinamfaa.
Ndio mnalojua tu hilo, jamaa ni Kiongozi haswa sitashangaa siku moja akiwa Rais wa nchi hii
 
Hersi awe mume wa utopolo wote Ndio cheo kinamfaa.
Leo nimemsikiliza huyu mgombea wa yanga jinsi kampun itakavokuwa baad ya yanga kuingia mfumo wa kisasa,, kwa mfano pale simba Mo alijipangia bei nakumbuka alitoa mpaka muda simba waamue kama hawataki hizo pesa pesa bilion 20 anaweza kununua Bank.

Yule muhindi ni tapeli, hebu soma jinsi yanga watakavoipata thaman halisi ya Club yao na uwekezaji utakavo kuwa.

“Asilimia 49 zimegawanywa kwa watu wanne tofauti ambao watakuwa na uwiano wa asilimia 12 kutoka taasisi au watu tofauti tofauti ambao vyanzo vya mapato hawashabiani kimapato kutakuwa na kampuni maalumu itakayofanya kazi ya kujua thamani ya klabu na wataweka wazi hadharani na mwenye uwezo wa kununua hisa atapata nafasi hiyo bila upendeleo wowote” - Injinia Hersi kuhusu uwekezaji ndani ya Yanga

Sisi mbumbumbu rage hakukosea kutubatiza hili jina,, leo hii mo anaweza kuamua kisusa tu na uwekezaji wake hewa na tutakarudi matopeni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…