Ajabu ya ligi daraja la kwanza uingereza "Championship "

Alvajumaa

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2018
Posts
5,039
Reaction score
6,253
Malimwengu!!! Mmeyasikia ya Leeds United na Aston Villa??? .....Achana na sare yao 1-1 iliyopelekea SHEFFIELD UNITED KUREJEA EPL!.... Kisanga ni namna goli hizo zilivyopatikana!...nitakusimulia!!! Kunako Dakika ya 73 mchezaji wa Aston Villa aliumia, ikatarajiwa mchezaji wa Leeds angetoa mpira nje kama sehemu ya FAIR PLAY! badala yake jamaa akatoa pasi LEEDS watapata goli la kuongoza!!!! REFA AKAMURU MPIRA KATI!......Kukaibuka vuta nikuvute wachezaji wa Aston villa wakimkunja Shati mfungaji aliyepotezea FAIR PLAY! ngoma ikawa Leeds 1-0 Villa!!! Kuona hivyo kocha wa LEEDS UNITED, MARCELO BIELSA AKAAMURU WACHEZAJI WAKE WASIKABE ILI ASTON VILLA WASAWAZISHE! Jamaa wakaanza wakapasiana na Kuscore! Ubao ukasoma 1-1....mechi ikaendelea na kuisha vivyo hivyo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Bielsa ni kocha makini sana. Tayari anajipanga kwa ajili ya play off games kwa "kuchagua" nani acheze naye. Ni hawa hawa Villa ama Derby
 
Hii sheria ya Fair play ibadilishwe maana Leeds walichokosea walifanya kama wanatoa mpira nje kumbe wakaenda kufunga sema sina hakika sana kama yule jamaa wa A villa aliumia kweli au alijifanya
 
Kama ni villa au derby basi atajipigia tu,cha msingi aendeleze tabia yake ya chabo,maana tangu ashtukiwe na kuacha,uongozi wa ligi ukamtupa mkono,natamani warejee.tangu mark viduka na smith nahodha radebe lucas si leo ati
 
Hii sheria ya Fair play ibadilishwe maana Leeds walichokosea walifanya kama wanatoa mpira nje kumbe wakaenda kufunga sema sina hakika sana kama yule jamaa wa A villa aliumia kweli au alijifanya
Wenger aliomba mechi irudiwe,mana kanu alipuyanga akaenda kufunga
 
leeds hiyo team sina bahati nayo kila nikimwamwini lazima aniangushe. alishawahi kunichania mkeka wa 600k, alipigwa kimoja ikashindikana kutoa ov 1.5
 
Malimwengu!!! Mmeyasikia ya Leeds United na Aston Villa??? .....Achana na sare yao 1-1 iliyopelekea SHEFFIELD UNITED KUREJEA EPL!.... Kisanga ni namna goli hizo zilivyopatikana!...nitakusimulia!!! Kunako Dakika ya 73 mchezaji wa Aston Villa aliumia, ikatarajiwa mchezaji wa Leeds angetoa mpira nje kama sehemu ya FAIR PLAY! badala yake jamaa akatoa pasi LEEDS watapata goli la kuongoza!!!! REFA AKAMURU MPIRA KATI!......Kukaibuka vuta nikuvute wachezaji wa Aston villa wakimkunja Shati mfungaji aliyepotezea FAIR PLAY! ngoma ikawa Leeds 1-0 Villa!!! Kuona hivyo kocha wa LEEDS UNITED, MARCELO BIELSA AKAAMURU WACHEZAJI WAKE WASIKABE ILI ASTON VILLA WASAWAZISHE! Jamaa wakaanza wakapasiana na Kuscore! Ubao ukasoma 1-1....mechi ikaendelea na kuisha vivyo hivyo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Huwezi kuta huu ujinga wamefanya ligi za spain...
 
Back
Top Bottom