Alvajumaa
JF-Expert Member
- Jul 5, 2018
- 5,039
- 6,253
Malimwengu!!! Mmeyasikia ya Leeds United na Aston Villa??? .....Achana na sare yao 1-1 iliyopelekea SHEFFIELD UNITED KUREJEA EPL!.... Kisanga ni namna goli hizo zilivyopatikana!...nitakusimulia!!! Kunako Dakika ya 73 mchezaji wa Aston Villa aliumia, ikatarajiwa mchezaji wa Leeds angetoa mpira nje kama sehemu ya FAIR PLAY! badala yake jamaa akatoa pasi LEEDS watapata goli la kuongoza!!!! REFA AKAMURU MPIRA KATI!......Kukaibuka vuta nikuvute wachezaji wa Aston villa wakimkunja Shati mfungaji aliyepotezea FAIR PLAY! ngoma ikawa Leeds 1-0 Villa!!! Kuona hivyo kocha wa LEEDS UNITED, MARCELO BIELSA AKAAMURU WACHEZAJI WAKE WASIKABE ILI ASTON VILLA WASAWAZISHE! Jamaa wakaanza wakapasiana na Kuscore! Ubao ukasoma 1-1....mechi ikaendelea na kuisha vivyo hivyo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]