Ajali kubwa duniani zilizowahi kutokea zilihusisha meli za mafuta

Ajali kubwa duniani zilizowahi kutokea zilihusisha meli za mafuta

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Hizi ni miongoni mwa ajali kubwa za meli za mafuta zilizowahi kutokea duniani na kuleta uchafuzi mkubwa wa mazingira ya bahari na athari kwa viumbe hai na watu waliozunguka maeneo hayo.

1.Torrey Canyon
SS Torrey Canyon ilikuwa meli kubwa ya mafuta saizi ya LR2 Suezmax na uwezo wa mizigo ya tani 120,000 za
mafuta ghafi. Ilivunjika meli kutoka pwani ya magharibi ya Cornwall, England, tarehe 18 Machi 1967, na kusababisha janga la mazingira. Wakati huo meli hii ilikuwa chombo kikubwa zaidi kilichopotea.

Ilikuwa na sifa hizi
Name: SS Torrey Canyon
Owner: Barracuda Tanker Corporation
Operator: British Petroleum
Port of registry: Liberia
Builder: Newport News Shipbuilding & Drydock Co
Yard number: 532
Laid down: 1959
Launched: 28 October 1958
Identification: UK official number : 536535
IMO number : 5365352
Fate: Sank after running aground on 18 March 1967
General characteristics
Type: Supertanker
Tonnage: 61,263 GRT
Length: 974.4 ft (297.0 m)
Beam: 125.4 ft (38.2 m)
Draught: 68.7 ft (20.9 m)
Propulsion: Single shaft; steam turbine
Speed: 17 knots (31 km/h; 20 mph)
Capacity: 120,000 tons of crude oil

Meli hii ilitengenezwa ikiwa na uwezo wa kubeba tani 60,000/= lakini baadae ikaongezewa uwezo huko Japan na kufikisha tani 120,000.

Meli hii ilizama katika pwani ya Uingereza baada ya kugonga Pollard rocks kati ya Cornish na visiwa vya Scilly tarehe ya 18 na meli ikaanza kuvunjika baada ya siku chache.
Serikali ya Uingereza ilichukua hatua kwa kutumia majeshi ya anga kwa kulipua meli kwa kutumia mabomu ili kupunguza kuenea kwa mafuta.
Royal Air Force(RAF) na Fleet Air Arm (FAA) walitumia mabomu 161, rocketi 16 na mafuta ya taa lita 44500 kulipua meli lakini mawimbi yalikuwa yakiupeleka kando mpaka meli yote ilipozama.

Kosa na chanzo cha ajali ya meli hii iliyosajiliwa nchini Liberia ilikuwa ni kosa la nahodha kupita njia nyingine na kuokoa muda ambapo alipita kwenye channel au mkondo ambao mshika usukani wa meli (helmsman) alikuwa amechelewa kubadili kutoka autopilot na wakati wanaingia eneo la mlango wa bahari.

Hii ajali ilileta athari kubwa sana na kupelekea aina nyingi za viumbe wa bahari kufa na watu wa maeneo ya karibu kuathirika kutokana na uchafuzi huu.
 
2.Amoco Cadiz
Hii ilikuwa ni meli kubwa ya mafuta ambayo ilipata ajali huko Portsall Rock kilometa 5 kutoka pwani ya Brittany nchini Ufaransa.

Mnamo tarehe 16/3/1978 ilitokea ajali hii na kusababisha meli hii kukatika sehemu 3 na kuzama kuliko sababisha mafuta tani 220880 kumwagika kwenye maji ya bahari.

Meli hii ilitoka Persian Gulf kuelekea Rotterdam na ilikuwa imepanga kusimama Lyme Bay Uingereza.

Wakati meli ikiwa kwenye safari eneo la English Chnanel( mkondo wa bahari wa Uingereza) ilipigwa na wimbi kali na kusababisha Rudder(kifaa kinachosaidia meli kukata kona) kutoweza kufanya kazi tena.

Ndipo meli ikaomba msaada wa Tug kutokana na meli kutokuwa na uwezo wa kufanya chochote kwenye kugeuka.

Msaada wa kusukumwa na Tug haukutosha kulingana na hali mbaya ya bahari, kamba za kuvutia zilikatika na ikaamuliwa Meli iangushe nanga lakini bado meli iliendelea kuzungushwa(Drift) na hali mbaya mpaka eneo la tukio.

Mnamo saa 3 usiku meli iligota na kuanza kumwagika mafuta. Muda huo mabaharia na nahodha walikuja kuokolewa na helicopta ya France Naval Aviation lakini ofisa mmoja alibaki ndani mpaka alfajiri ya saa 11 alipokuja kutolewa.

Athari zake ilichafua maeneo ya fukwe kilometa kama 72 na ilisababisha mafuta kuingia kwenye mchanga wa beach sentimenta 50. Hii ulikuwa ukichimba nusu mita unakutana na mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye meli.

Hii ni moja ya ajali za meli za mafuta zilizoleta athari kubwa sana kwa viumbe wa baharini kama samaki,ndege na kobe.

Hii ilikadiriwa kuleta maafa yalifikia thamani ya dola million 250 za kimarekani kwenye masuala ya uvuvi na makazi ya kitalii kwenye fukwe.
Mwisho mwaka 1992 kampuni kubwa ya kimarekani ya Amoco ilikata rufaa na kudai kulipa dola million 200 kama fidia kwa madhara yaliyotokea.
 
Amoco Cadiz ilikuwa imesajiliwa nchini Liberia ila wamiliki ni kampuni ya Marekani.
Amoco-Cadiz.jpg
 
Nini kilitokea kwenye Gulf of Mexico hadi Shell ya Uholanzi almanusra wafilisike?
Hili tukio linaitwa Deepwater Horizon oil spill ilitokea ajali kwenye oil rig iliyosabaisha kumwagika kwa mafuta na kutokea mlipuko mkubwa.
Ilikuwa mnamo mwaka 2010 hii ilikuwa ni kwenye ule mtambo wa kuchimba mafuta baharini (Oil Rig).
 
Hizi ni miongoni mwa ajali kubwa za meli za mafuta zilizowahi kutokea duniani na kuleta uchafuzi mkubwa wa mazingira ya bahari na athari kwa viumbe hai na watu waliozunguka maeneo hayo.

1.Torrey Canyon
SS Torrey Canyon ilikuwa meli kubwa ya mafuta saizi ya LR2 Suezmax na uwezo wa mizigo ya tani 120,000 za
mafuta ghafi. Ilivunjika meli kutoka pwani ya magharibi ya Cornwall, England, tarehe 18 Machi 1967, na kusababisha janga la mazingira. Wakati huo meli hii ilikuwa chombo kikubwa zaidi kilichopotea.

Ilikuwa na sifa hizi
Name: SS Torrey Canyon
Owner: Barracuda Tanker Corporation
Operator: British Petroleum
Port of registry: Liberia
Builder: Newport News Shipbuilding & Drydock Co
Yard number: 532
Laid down: 1959
Launched: 28 October 1958
Identification: UK official number : 536535
IMO number : 5365352
Fate: Sank after running aground on 18 March 1967
General characteristics
Type: Supertanker
Tonnage: 61,263 GRT
Length: 974.4 ft (297.0 m)
Beam: 125.4 ft (38.2 m)
Draught: 68.7 ft (20.9 m)
Propulsion: Single shaft; steam turbine
Speed: 17 knots (31 km/h; 20 mph)
Capacity: 120,000 tons of crude oil

Meli hii ilitengenezwa ikiwa na uwezo wa kubeba tani 60,000/= lakini baadae ikaongezewa uwezo huko Japan na kufikisha tani 120,000.

Meli hii ilizama katika pwani ya Uingereza baada ya kugonga Pollard rocks kati ya Cornish na visiwa vya Scilly tarehe ya 18 na meli ikaanza kuvunjika baada ya siku chache.
Serikali ya Uingereza ilichukua hatua kwa kutumia majeshi ya anga kwa kulipua meli kwa kutumia mabomu ili kupunguza kuenea kwa mafuta.
Royal Air Force(RAF) na Fleet Air Arm (FAA) walitumia mabomu 161, rocketi 16 na mafuta ya taa lita 44500 kulipua meli lakini mawimbi yalikuwa yakiupeleka kando mpaka meli yote ilipozama.

Kosa na chanzo cha ajali ya meli hii iliyosajiliwa nchini Liberia ilikuwa ni kosa la nahodha kupita njia nyingine na kuokoa muda ambapo alipita kwenye channel au mkondo ambao mshika usukani wa meli (helmsman) alikuwa amechelewa kubadili kutoka autopilot na wakati wanaingia eneo la mlango wa bahari.

Hii ajali ilileta athari kubwa sana na kupelekea aina nyingi za viumbe wa bahari kufa na watu wa maeneo ya karibu kuathirika kutokana na uchafuzi huu.
Hivi kwa nini Meli nyingi za mizigo zimesajiliwa Liberia?
 
Hivi kwa nini Meli nyingi za mizigo zimesajiliwa Liberia?
Liberia ni miongoni mwa nchi zinazofanya usajili wa meli aina ya Open registry au Flag of Convenience ambapo mtu yeyote ambaye si raia wa Liberia anaruhusiwa kusajili meli yake.

Wamiliki wengi wa meli za mizigo wanapenda kusajili kwenye nchi kama hizi ili kupata nafuu ya kodi,uhuru wa kusajili popote na sheria za kawaida kutoka nchi husika.
 
Hapo kwenye ku control spill kwa kulipua ndo sijaelewe. HOW??
Mafuta baada ya kumwagika kwenye maji walimwaga mafuta ya taa na kulipua ili mafuta ghafi kutoka kwenye meli yaweze kuungua na yasibaki tena kwenye maji.

Pia walitumia vilipuzi kama mabomu na roketi ili mafuta ghafi yanayoelea yaungue baada ya mlipuko wa bomu.
 
Back
Top Bottom