The Rookie
New Member
- Dec 6, 2024
- 4
- 4
Leo, Disemba 6, 2024, basi lililokuwa limebeba wabunge waliokuwa wakielekea kwenye mashindano ya michezo ya Mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki limepata ajali katika eneo la Mbande, Kongwa, mkoani Dodoma. Kwa mujibu wa Polisi mkoani Dodoma, ajali hiyo ilitokea baada ya dereva wa basi kujaribu kulipita lori lililokuwa mbele yake, ambapo basi hilo liliishia kugonga lori hilo kwa nyuma.
Licha ya tukio hili kuwa wazi, jambo linaloshangaza ni jinsi baadhi ya vyombo vya habari nchini, hususan vile vinavyochukuliwa kama 'vyombo vya kuaminika', vilivyotoa taarifa zisizo sahihi kwa kusema kwamba "basi lililowabeba wabunge limegongana na lori", huku ukweli wake ukiwa ni "basi lilowabeba wabunge limegonga lori"
Kosa hili, lililofanywa na baadhi ya vyombo vikubwa vya habari, linazua maswali makubwa kuhusu jinsi habari zinavyotolewa, hasa pale zinapohusu watu wa mamlaka. Mambo makuu matatu yanajitokeza:
PIA SOMA
- News Alert: - Dodoma: Basi lililobeba Wabunge wa Tanzania lagonga Lori na kuwajeruhi Wabunge kadhaa
1. Kipaumbele kwa 'Breaking News' Badala ya Ukweli
Inaonekana vyombo hivi vilikimbilia kuandika habari ili kuwa wa kwanza kufikisha taarifa kwa umma (breaking news) badala ya kufanya uhakiki wa kina (fact-checking). Hii ni dalili ya changamoto kubwa katika tasnia ya habari ambapo shinikizo la ushindani wa muda wa kufikisha habari linatuzidi uhitaji wa usahihi. Picha za tukio, zilizochapishwa na ukurasa rasmi wa Bunge, zilionyesha wazi kuwa basi lililogonga lori kutoka nyuma, lakini taarifa sahihi hazikupewa uzito.
2. Censorship na Hofu ya Kukosoa Watawala
Hofu iliyopo kuhusu ukosoaji wa mamlaka inaweza kuwa sababu ya ripoti hizi zilizopindishwa. Inawezekana vyombo hivi vilijikuta vikifanya self-censorship, wakiepuka kusema ukweli kuwa basi lililobeba wabunge ndilo lililosababisha ajali kwa hofu ya kuonekana wanakosoa watu walioko madarakani. Hofu kama hii inaweza kuathiri sana uhuru wa vyombo vya habari na kuzidi kudhoofisha uaminifu wa habari zetu.
3. Kutumika kwa Vyombo vya Habari Kama Vyombo vya Propaganda
Kuna uwezekano kuwa vyombo hivi viliridhia kupotosha ukweli kwa ajili ya kulinda maslahi ya watawala. Dhana ya "baba hakosei" imetamalaki sana katika mfumo wetu wa uongozi, ambapo mamlaka zina kinga dhidi ya uwajibikaji. Hili linaweza kuchangia vyombo vya habari kuripoti habari potofu ili kuficha makosa ya watawala au taasisi zao.
Binafsi, nadhani upotoshaji wa habari wa namna hii una madhara makubwa kwa wananchi wa kawaida. Kwa jamii inayotegemea habari sahihi kwa ajili ya kufanya maamuzi, upotoshaji wa aina hii unawanyima fursa ya kuelewa ukweli wa matukio na kufanya maamuzi yanayofaa.