Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

Watu

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2008
Posts
3,231
Reaction score
1,471
Kuna ajali mbaya sana imetokea Ihemi maeneo ya Iringa karibu na kijiji cha Ifunda ambayo inamhusisha Dr. Mwakyembe

Taarifa zaidi zinafuatia:

Picha ni hizi


Dr Mwakyembe akifikishwa hospitali ya mkoa wa Iringa leo baada ya ajali


Gari la Dr Mwakyembe likiwa limeharibika vibaya baada ya ajali


Shimo lililosababisha ajari ya Dr Mwakyembe

UPDATES:

REPORT YA MWAKYEMBE:

Hii hapa chini ni taarifa ya Dk Mwakyembe ambayo ameituma kwenye kampuni ya Guardian Limited baada ya kuona hata jeshi la polisi limeingia kwenye upotoshaji

 
Last edited by a moderator:
Confirmed. Dr Mwakyembe amepata ajali mbaya Ifunda na amelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa. Hajitambui na Madaktari wanafanya kila wanaloweza kumsaidia. Taarifa kamili ya maendeleo ya hali yake mtaipata baadae maana nipo eneo la hospitali. Wakati huu tumuombee kwa Mungu apate nafuu.
 
Mungu amsaidie apate kupona haraka! We need him now more than ever!
 
Thank God. Alikuwa amepata shock ya ajali na sasa amezinduka. Madaktari wametuondoa hofu kuwa hana majeraha makubwa. Wanasubiri vipimo kufanya uchunguzi zaidi kabla hawajamruhusu kutoka.
 
Duh ni ajali ya kawaida au ndo hivyo tena yale yale?
Lakini eneo hilo kwa ajali linatisha sana magari mengi yanapata ajali eneo hilo.
Tunamwombea apone haraka
 
Mungu amjalie apone haraka mpiganaji wetu.
 
Mmmhhh!!! ajali tena? Pole sana kwa Dr. Mwakyembe pamoja na familia yake. Mungu amsaidie apate nafuu mapema.
 
Amezinduka...Ameumia taya...Hayuko hatarini...Vibaka wamewaaibia kila k2...dereva wake ameumia vibaya...
 
Thank God. Alikuwa amepata shock ya ajali na sasa amezinduka. Madaktari wametuondoa hofu kuwa hana majeraha makubwa. Wanasubiri vipimo kufanya uchunguzi zaidi kabla hawajamruhusu kutoka.

Yuko wodi gani?
 
Pole sana Kamanda, Nakutakia upone haraka!
 
Tumuombee kila la kheri apone haraka, siku zote watu wazuri kwa jamii ndiyo hupata misuko suko kama hii. Bila shaka RA na EL watafurahi.

Je, tunaweza kujua ajali imetokeaje?
 
Tunamwombea, Mungu amjalie apone...tunamhitaji sana mpiganaji wetu
 
Mpole mheshimiwa Dk mwanajeshi wetu, Mungu atakusaidia bado tunakuhitaji kazi baado baba...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…