Ajali ya gari na Nyambizi miaka 60 iliyopita

Ajali ya gari na Nyambizi miaka 60 iliyopita

Polycarp Mdemu

Senior Member
Joined
Jun 2, 2019
Posts
165
Reaction score
209
Siku kama ya leo miaka 60 iliyopita Kwa mara ya kwanza Gari aina ya Volvo PV444 na Nyambizi iliyoitwa Hayen III ziligongana.

Ajali hii ilitokea Mjini Liskill huko Sweden, mwaka 1960, hii ilikuwa mara ya kwanza na ya mwisho kutokea ajali kama hii.

Gari hili lilikuwa limeegeshwa mbele ya banda la simu kwenye Mtaa wa Fiskaregatan. Kwa sababu isiyojulikana gari ambalo hakukuwa na mtu ndani yake lilianza kushuka chini kuelekea baharini.

Baada ya kukatisha salama shehena kubwa ya mapipa ya siagi ambayo yalikuwa yamepakuliwa tu kutoka katika meli iliyotoka nchini Iceland

Gari lilivuka Barabara ya Södra Hamngatan kando ya bahari na kugonga upinde wa nyambizi

Sehemu ya mbele ya gari katika ajali hiyo ilikandamizwa, Na katika nyambizi ile ikaonekana kuwa na michubuko yenye kufuatana Hakukuwa na mtu aliyeumia.

Nyambizi ile iliendelea na huduma yake hadi mwaka 1980, baada ya hapo ilisimama kazi na mwaka uliofuata ikakatwa vipande kwa chakavu huko mjini Odense, Hatima zaidi ya gari haijulikani.

Polycarp Mdemu


FB_IMG_1629215723223.jpg
 
Back
Top Bottom