Ajali za barabarani, ukweli huu unapuuzwa?

Ajali za barabarani, ukweli huu unapuuzwa?

Mtu_Mzima

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2014
Posts
1,164
Reaction score
1,134
Kujadili hoja yangu nitajikita kwenye maeneo haya:

1. Mafunzo ya udereva
  • Hivi kweli tunaweza kusema kuna mafunzo ya udereva hapa chini?
  • Je, tuna mtaala (sylubus) ya mafunzo ya awali ya udereva?
  • Je, tuna mafunzo ya waalimu wa shule za udereva?
  • Nani anaangalia umahiri wao?
  • Wanafunzi wanakaa muda gani darasani na barabarani?
  • Haya magari ya mafunzo si yale mabovu kabisa?
  • Yamewahi kukagukiwa?
  • Yana vehicle inspection report?
  • Hivi serikali inajua mpaka leo, pomoja na wingi wa pikipiki, bajaji, malori hakuna shule ya udereva wa awali wa vyombo hivyo?
  • NIT wao ili wakupokee ni lazima uwe na leseni ya daraja C, E nk
  • Kwa sasa shule kuu ya udereva ipo mtaani, malori ni utingo..pikipiki ni kijiweni nk
2. Upatikanaji wa leseni za udereva
Mara ya mwisho au ni nani amewahi kumuona mtu yupo barabarani na trafiki,vehicle akimjaribu kabla ya kumuidhinishia leseni?

Yanayotokea huko NIT ili ufaulu practical yanajulikana kwa wote waliopitia. Madalali wa leseni polisi na TRA ni kama wote. Ukienda mwenyewe kufuatilia unaonekana mnoko...unaulizwa...huna vijana? Kama huna tukupe namba !!![emoji87]

3. Modifications kwenye magari
Fuso nyingi zina mfumo unaitwa "tandam". Huu wa kuongeza exeli ili kuongeza mzigo. Hizi modifications zinaathiri mfumo wa brake na centre of gravity. Na ukichanganya na mzigo uliobebwa gari haiwezi kusimama ghafla. Pia kuna mfumo wa " mende". Yote hii huharibu uhalisia wa gari. Haya yanatakiwa yatolewe kauli baada ya tathmini ya kina badala ya kuhangaika na ving'ora tu muda wote.

4. Kuchezea mfumo wa taa
Upo mchezo sasa wa kufunga buster na kumodify taa za mbele ili kuziongezea mwanga uwe mkubwa.
Ukipishana na magari mengine usiku utajiuliza kama huyu dereva yupo sawa. Nao wanawasha, hata ukimtaka apunguze hapunguzi. Wengine wanaongeza na sport lights. Hili lijumuishwe kwenye ukaguzi.

5. Ubebaji wa mizigo uliozidi
Michezo ya mizani ni kama kawaida. Huwezi jua lori na basi. Nyomi kila kona. Magari mengi yanabeba zaidi ya uzito sahihi. Hapa tajiri akitaka ugomvi na dereva adai karatasi za mizani.

6. Hali ya barabara zetu
Shetia na kanuni za LATRA zinamtaka deteva apumzike baada ya masaa 8 au 10 kama bado anaendelea na safari. Barabara zetu zina stendi ya kushushia abiria tu. Hakuna mahali pa lori kupumzika na kufanya ukaguzi, hakuna mahali pa kumpumzika abiria kama sio hotelini. Ubovu wa barabara zetu na wembamba unafanya udereva uwe mgumu haswa usiku.

7. Kero ya polisi wetu
Huwezi kuwajua polisi wetu mpaka upande lori kuelekea popote. Hakuna lori linalompita polisi. Lazima asimamishe, na hii imewafanya madereva wengi kuamua kusafiri usiku maana mchana hakufai. Naona na magari madogo yameamua nayo kuhamia usiku sababu ya hizi tochi za kushtukiza/kubambikia. Unasimamishwa kwa mwendo kasi na ukimwomba akuonyeshe hana kisa gari zuri..lazima atakuwa amekimbia huyu. Jamani!

8. Tunahitaji mjadala wa kitaifa ili wale wa kuambiwa waambiwe na pale pa kutengeneza upya tukumbaliane.
Hili la ukaguzi, operesheni, ni kuongezeana ulaji, hakutatatua tatizo.
 
Mkuu ujuzi wa barabarani ni ku practice.... ukiweka kama unavyotaka sidhan kama kuna atakeweza.. kwani hata degree na masters hata phd bila practice ni ujinga tu.

Cha muhim useme sheria ziwe kali... hasa kwa hao boda, bajaj, buss, na malory hasa mafuso... mirungi, bange nyagi na driving wap ma wap.
 
Back
Top Bottom