Ghost MVP
JF-Expert Member
- May 19, 2022
- 439
- 736
Hivi karibu kumekuwa na Ajali nyingi za ndege ambazo zimechukua uhai wa watu wakubwa Duniani, imefika mahala jamii inatilia Shaka Uhalisia wa ajali hizi hasa kwa viongozi fulani.
Tujikumbushe Kidogo baadhi ya Viongozi waliofariki katika ajali Hizi za ndege katika maeneo Tofauti.
1. Yevgeny Prigozhin (Kiongozi wa Wagner Group) Agosti 23, 2023
Alikuwa Mhasimu mkubwa wa rais wa Rusia (Putin), Baada ya kuonesha nia ya kutaka Kumpindua kwa mabavu baada ya Putin kutoka kauli zilizomkwaza Kiongozi huyo wa Kundi la Wapiganaji wa Kulipwa, Kiongozi huyo ambaye alikuwa na Kundi la wapiganaji 50,000 (Kulingana na data za 2022 United States National Security Council Coordinator for Strategic Communications John Kirby)
Chanzo cha ajali kilichoripotiwa ni "pilot error"
2. Ebrahim Raisi (Rais wa IRAN) Mei 19, 2024
ALiyekuwa Rais wa IRAN kwanzia mwaka 2021 hadi umauti ulipomkuta katika Ajali ya Ndege 2024. Tukio hili limetokea siku chache baada ya Kutoa kauli dhidi ya ISRAEL aliyosema "Nothing will be left be left of israel if it again attacks IRAN"(Hakuna kitakachobakia Israel kama itaishambulia Tena Iran
Kwa kipindi hiko ISRAEL ilikuwa kwenye vita na HAMAS na HEZBOLLAH, ambapo Raisi EBRAHIM aliipiga Israle kwa Makombora ya masafa marefu(Rockets) baada ya kuituhumu Israel kushambulia Ubalozi wake uliopo Damascus na Kuua watu 7 akiwemo Jenerali wa Jeshi la Iran. Alichofanya Rais IBRAHIM ni kama kulipiza kisasi na kuonya Israel kama Itarudisha mashambulizi basi ndo utakuwa Mwisho wao
Chanzo cha ajali ni Itilafu ya Injini
3. Jenerali Francis Ogolla (Mkuu wa majeshi ya Kenya) Aprili 18, 2024
Alikuwa Mkuu wa Majeshi ya Kenya tangu alipochukua nafasi hiyo Aprili 28, 2023 hadi umauti ulipomkuta. Alifariki na Ajali ya ndege Iliyotokea Aprili 18, 2024 baad aya Kutoka eneo la kaben, Marakwet.
Rais Ruto alimpandisha cheo Luteni Jenerali Francis Omondi Ogolla kuwa Jenerali na kumteua kuwa CDF akichukua nafasi ya Jenerali Robert Kariuki Kibochi aliyemaliza muda wake
Chanzo cha ajali ni hitilafu ya Injini
4. Dkt. Saulos Chilima (Makamu wa Rais wa Malawi) Juni 10, 2024
alikuwa makamu wa Raisi nchini Malawi mwaka 2024 hadi 2019 na akaingia tena 2020 hadi kifo kilipomkuta, Tetesi zinasema Walikuwa na makubaliano na Raisi wa Nchi hiyo kuwa awamu hii yeye ndiye atagombania kama Raisi, ambapo uchaguzi unatarajia kufanyika Septemba 2025.
Ndege yake Ilipotea Ghafla Kwenye rada baada ya kushindwa kutoa kutokana na hali ya hewa na kulazimika kugeuza, lakini dakika chache baada ya kugeuza ilipotea na kuja kupatikana siku mbili badae ikiwa imepata ajali katika Milima na kuuwa watu zaidi ya 9
Chanzo cha ajali Hitilafu ya Injini