Njaa, mbaya sana na kushikwa masikio na mameneja uchwara .
Ajibu angesubiri mkataba wake uishe aangalie ofa zitakazokuja mezani kwake kulingana na jasho na damu alilolitoa kuudhihirishia umma kuwa anajua soka.
Kafanya kazi kubwa, akiwa Yanga kila mdau wa soka akajiridhisha kijana amepambana ndo maana wale wenye mawazo ya soka la kizamani la "KUKOMOANA"
Walipoona ili uidhoofishe Yanga msajili Ajibu ili wakose zile assist zake na faulo za hatari, ukichanganya na njaa ya meneja na mchezaji unategemea nn?
Nakumbuka maneno ya rais wa muda wa Simba "TRY AGAIN" huyu ni kiongozi shupavu, aliweka wazi wakati Yondani anasuasua kusajili Yanga, alisema "HATUUSAIDII MPIRA WETU" tukimsajili Yondani ni kuididimiza Yanga.
Angalia Yanga wamemsajili Ajibu na Simba tumemsajili Niyonzima ! Kipi kilichopatikana ? Kwa maendeleo ya mpira wetu zaidi ya KUKOMOANA na kujirudisha nyuma.
Ajibu , kama angevumilia Njaa, Mkataba wake ungeisha na kwenda Tp Mazembe ambako angeweza kukutana na changamoto mpya na watu tofauti wenye jicho halisi la kipaji cha soka, huenda angefanikiwa sana.
Kwa hapa Bongo, sioni Ajibu akichanua kiwango naona kimefika Peak akiwa Yanga, ambako alikuwa anacheza kila siku. Simba kiwango kinarudi chini kwa kukosa nafasi.
Ajibu jitafakari Omba kwenda kucheza kwa mkopo kwenye timu kama, Mtibwa, Kagera, Namungo au Azam. Pandisha kiwango SONGA MBELE.