Ajibu Vs Nyoso

Anselm

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2010
Posts
1,710
Reaction score
291
Kabla mechi ya Yanga na Kagera haijapigwa kule Kaitaba Jumamosi iliyopita,mmoja wa mabeki anayesifika kwa kukaba mpaka kivuli na ki'ukauzu kabisa Juma Saidi Nyoso alijinasibu kuwadhibiti washambuliaji wa Yanga haswa Ibrahimu Ajibu aka Fundi aka Miguu ya dhahabu,nafikiri Nyoso alijiaminisha kuwa Ajibu atakuwa kama Mhenga John Boko ambaye aliwahi kumficha kwenye mechi kadhaa...
Tofauti na matarajio yake,alichokipata katika mchezo ule hatakuja kukisahau katika kipindi chote atakachocheza mpira...

Kwanza alianza kwa kumvuta ili ajae vizuri [emoji23] [emoji23].

Alivyojaa vizuri akala tobo 1 matata sana[emoji23] [emoji23] [emoji23].
Ikapita,ikaja move nyingine...

Akazungukwa [emoji23] [emoji23].
Mzee mzima akaona isiwe tabu,akarudi zake golini kwenda kukaba wachezaji wengine.
Ikaja move nyingine...
This time akaamua kuingia na Mibange yake...

Akapigwa chenga 1 maridhawa kabisa [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Dah mtu mzima akaona huku sasa ni kudharirishana,faster akageuka ili amvute jezi...
...jezi akaikosa,akataka auwahi mkono,nao akaukosa [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Huyu ndo Ibrahim Ajibu Migomba aka Fundi,aka Miguu ya dhahabu.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hivi miguu inayompiga tobo "babu" Nyoso inageuka na kua ya dhahabu? Mfikishieeni taarifa "loo betri" kua Baba Mwenye Nyumba na "General" Juko wanamsubiri kwa hamu.
 
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€Huo sasa ni unyanyasaji...Ajibu sio fresh ujue??
 
Hivi miguu inayompiga tobo "babu" Nyoso inageuka na kua ya dhahabu? Mfikishieeni taarifa "loo betri" kua Baba Mwenye Nyumba na "General" Juko wanamsubiri kwa hamu.
Sasa kama ni issue ya U'babu mbona huyo mnayemuita Baba Mwenye nyumba hana mpinzani katika ukanda wote huu wa Africa Mashariki?
 
Sasa kama ni issue ya U'babu mbona huyo mnayemuita Baba Mwenye nyumba hana mpinzani katika ukanda wote huu wa Africa Mashariki?

Mkuu nadhani hujanielewa.. Mimi nimeandika "babu" na si babu.. Ambayo ni maneno mawili tofauti.. ukitaka kufahamu tofauti yake karibu Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…