Ajifanya Mkuu wa Wilaya na kutapeli viwanja Homboza, Kisarawe

Ajifanya Mkuu wa Wilaya na kutapeli viwanja Homboza, Kisarawe

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mtu mmoja (jina limehifadhiwa) anadaiwa kufoji nyaraka na kujifanya mwakilishi wa mmoja wa Wakuu wa Wilaya waliowahi kuongoza Wilaya ya Kisarawe, akidai kuuza viwanja kwa niaba ya mkuu huyo wa wilaya aliyepita.

Tuhuma hizi zilibainishwa na Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Petro Magoti, wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Homboza kwenye mkutano wa hadhara uliohusisha kamati ya ulinzi na usalama pamoja na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe. Mkutano huo ulilenga kusikiliza changamoto za migogoro ya viwanja kijijini hapo.

DC Magoti ameeleza kuwa alipompigia simu mkuu huyo wa wilaya aliyepita, alikanusha kumiliki viwanja eneo la Homboza wala kumtuma mtu yeyote kuuza viwanja kwa niaba yake.

Aidha, amewataka wananchi kuwa makini na kuhakikisha wanafuata njia rasmi za upatikanaji wa viwanja ili kujikinga na hasara zinazoweza kusababishwa na vitendo vya ulaghai.

 
Back
Top Bottom