Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Mwanaume mmoja ajulikaye kwa jina la Marco Samweli mwenye umri wa miaka 32 mkulima na mkazi wa Kijiji cha Kibitilo kata ya Ilula wilayani Kwimba mkoani Mwanza amejikata uume wake na kisha kuutupa kwa kutumia kisu kwa madai kuwa amechoka kuumwa ugonjwa uliokuwa unamsumbua.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza Wilbroad Mutafungwa amesema tukio hilo limetokea may 5 mwaka huu majira ya saa saba usiku mara baada ya mwanaume huyo kutoka hospitali kwa maradhi yanayomsumbua ambapo inadaiwa aliugua kwa zaidi ya miaka mitano.
Aidha kamanda Mutafungwa amesema kwa sasa mgonjwa huyo anatibiwa katika hospitali ya rufaa ya kanda Bugando akiwa chini ya ulinzi wa jeshi hilo kutokana na kitendo alichofanya cha kujijeruhi na pindi atakapopona jeraha lake atafikishwa mahakamani kujibu shtaka linalomkabili.
Manara TV