Ajinyonga kwa kukatazwa kuoa mke wa pili

Ajinyonga kwa kukatazwa kuoa mke wa pili

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Posts
3,068
Reaction score
277
MKAZI wa kijiji cha Ubinga kata ya Mhugi, Tabora, Bundala Mwandu (26) amejinyonga baada ya walezi wake kumkataza kuoa mke wa pili.

Akithibitisha jana kutokea kwa tukio hilo, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Nzega, Issa Muguha, alisema Mwandu alikutwa amejinyonga Juni 13 saa nne asubuhi katika kijiji hicho.

Muguha alisema, kabla ya kujinyonga, Mwandu alikuwa na mke mmoja na alitaka kuoa wa pili, lakini alipopeleka taarifa hiyo kwa walezi wake, hawakukubaliana na uamuzi huo.

Baada ya taarifa hiyo kukataliwa, Mwandu alifikia uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ya gome la mti.

Akizungumza na gazeti hili, babu wa Mwandu, Bulabo Kinimba, alisema alipopata taarifa ya mjukuu wake kutaka kuoa mke wa pili, alimshauri asubiri mpaka baadaye.

Kinimba alisema alimshauri kwamba kwa sasa umri wake hauruhusu kubeba majukumu makubwa ya familia mbili.

“Nilimwambia asubiri baadaye ndipo angeze mke wa pili, kwani bado ana umri mdogo, nashangaa kijana wangu amefikia uamuzi huu,” alisema babu huyo.
 
26 yrs na mke mmoja hamtoshi!!!!?
mmh, kazi ipo!!

ee Mwenyezi Mungu, tusaidie
 
Hata huko alikofikia atakuwa amejinyonga bila shaka. Pumbavuuu sanaaa!
 
huyu bwana kanishangaza sana, cjawah ona zoba kama hili duh! Iyo ya huyo waliemzuia ilikua ina AC?
 
26 yrs na mke mmoja hamtoshi!!!!?
mmh, kazi ipo!!

ee Mwenyezi Mungu, tusaidie

Hahahahah dah,

Off topic, Miss Judith tunaomba majibu coz siku 30 zimeshapita sasa vipi mambo yapoje mbona hutushirikishi wana MMU tuliokuwa tunakuombea! Jamaa vipi anashangilia mida hii au hajaona ndani hadi mida hii?
 
Kweli tunatofautiana,wengine wanakua mwili ila siyo akili
 
hata kama alionjeshwa yenye ac,atajibeba sasa. mkewe karudi kwenye market sasa, asifanye makosa! kama kuna anaemjua mjane amuelekeze aje aanzishe uzi hapa chap chap achangamkie tenda kungali mapemaa!
huyu bwana kanishangaza sana, cjawah ona zoba kama hili duh! Iyo ya huyo waliemzuia ilikua ina AC?
 
Back
Top Bottom