Ajira bomba la mafuta zaanza kutangazwa

Ajira bomba la mafuta zaanza kutangazwa

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Zile ajira takribani 10,000 ambazo Watanzania waliahidiwa kunufaika nazo katika ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika mashariki (EACOP) kutoka Hoima Uganda handi Chongoleani Tanga zimeanza kutangazwa.

Kupitia gazeti la Mwananchi toleo namba 0856-7573 la Jumatatu, 26/07/2022 ajira 87 za moja kwa moja zimetangazwa ambazo Watanzania wamehimizwa kuomba nafasi hizo kabla ya Agosti 8 mwaka huu.

Miongoni mwa nafasi zilizotangazwa na kampuni ya FABEC Investiment Ltd mkandarasi msaidizi anayejenga kiwanda cha kuborsha mfumo wa joto la mambomba kati ya yadi iliyopo kata ya Isugule, wilayani Nzega Tabora, zipo nafasi za msimamisha chuma, mnyanyuzi, mrekebisha chuma, fundi ujenzi, fundi seremala na meneja rasilimali watu.

Aidha mratibu wa mradi huo ameeleza katika maeneo ambayo mradi huo unapita tayari Watanzania 180 wameshaajiriwa lakini kutokana na ukubwa wa mradi ni ngumu kuwa na takwimu za jumla za Watanzania ambao wamekwishapata ajira lakini ameeleza kuwa kadiri siku zinavyokwenda Wakandarasi wanatarajiwa kuajiri Watanzania 6,000 kati ya 10,000 wanaotarajiwa kupata ajira.

Tuchangamkie fursa hizo

Chanzo: Mwananchi

Mafuta.jpeg
 
Nikiwa fundi ujenzi wa kawaida Sina vyeti napataje kazi huko
 
Walianza kutangaza ajira muda kidogo, isipokuwa ilikuwa kwa nafasi chache...
 
Ila hii miradi inayotegemea hela za wafadhiri ambao wana mpango wa kutemana na fossil fuels ni mtihanj
Ila naona bado unasonga, japo fossil fuel inapigwa sana vita
 
Na mpaka leo vita za chinichini zinaendelea
Wakenya wajinga sana! Siyo wa kuwachekea hao. Wameng'ang'ana mno na uchafuzi wa mazingira kumbe ni wivu tu kwa vile mradi ulihamishwa kutoka nchini kwao! Huu ungekuwa kwao wala kelele zisingekuwapo!
 
Back
Top Bottom