Ajira, elimu na afya: Je, tusiiamini Serikali yetu?

mom abe

Member
Joined
Jun 13, 2024
Posts
17
Reaction score
19
Toka mwaka jana Serikali iliahidi kutoa ajira kadhaa kwenye sekta ya afya na elimu, kati ya mwezi wa kwanza au wa pili na haijawa, katika bunge la bajeti waziri akaahidi kabla ya June 31 ajira zitakuwa zimetolewa ila hadi leo mwaka mwingine wa fedha umeanza bado kimya.

Je, kama hawakuwa na mpango kwanini watoe ahadi za uongo? Hawaoni wanaharibu akili za wahanga wa ajira, ambao tuna karibia miaka kumi mitaani?
 
Tunatafuta kazi Hadi tunachoka 😥😥 sijuh wengine wanapataje
Wana moto wao special kabisa siku ya kiama hao watu...na ukute hizo ajira walizoahidi saiz zinagawanwa Kwa watu wao na Koo zao Hadi ziishe wakihakikisha Kila ndugu Yao kapata ndo wanatangaza kama ushahidi 🤣
 
Bora usiziwaze hizo ajira kuliko ukaanza kuziwazia kabla za hazijatoka alafu zikitoka unakosa maumivu yake Huwa ni makubwa mno.
 
Ni kweli ila ahadi za uongo zinatufanya tukose imani na taarifa zinazotolewa na serikali
 
Serikali yetu tukufu sijuwi huwa inatuchukuliaje tu. Yaani
 
Toka mwaka jana Serikali iliahidi kutoa ajira kadhaa kwenye sekta ya afya na elimu, kati ya mwezi wa kwanza au wa pili na haijawa, katika bunge la bajeti waziri akaahidi kabla ya June 31 ajira zitakuwa zimetolewa ila hadi leo mwaka mwingine wa fedha umeanza bado kimya.

Je, kama hawakuwa na mpango kwanini watoe ahadi za uongo? Hawaoni wanaharibu akili za wahanga wa ajira, ambao tuna karibia miaka kumi mitaani?
Pole sana kama bado unawaamini wanasiasa wa Afrika
 
Back
Top Bottom