ItsMi
Member
- Sep 13, 2021
- 66
- 31
Habari yako mdau unaefwatilia makala hii
Siku ya leo karibu tuangazie mambo yanayolenga ukatili wa kijinsia katika maeneo ya kazi
Karibu
Mdau wangu kama unavyofahamu kwamba kwa hivi sasa kuna tatizo kubwa sana la watu kupata ajira na hii inatokana au kusababishwa na utandawazi unaokua kwa kasi mno katika maeneo yaliyo mengi.
Sasa hivi uwepo wa vifaa mbalimbali vya kielektroniki imepelekea kwamba kazi nyingi zimerahisishwa ambapo inaweza kuwa kompyuta ikafanya kazi zilizokuwa zinafanywa na zaidi ya watu sita badala yake kazi hiyo ikafanywa na mtu mmoja kwa kuongoza kompyuta hiyo.
Sasa inamaana ajira zinakuwa ndogo la sivyo uwe mbobevu wa kuzitambua fursa ili uweze kujiajiri wewe mwenyewe.
Lakini watu wengi wamekuwa na tumaini la kuajiriwa katika maeneo mbalimbali badala ya kujiajiri ili waweze kujipatia ujira wao
Hata hivyo zimekuwepo changamoto kubwa sana kwa wale wanaotafuta ajira hasa jinsia ya kike ambapo anamkuta bosi akimtaka kimapenzi na kumuahidi kwamba atampatia ajira au kumpandishia mshahara endapo tu atakubali kuwa naye katika mahusiano hayo ambapo kwa huyo mwanamke ambaye ndiye anatafuta nafasi ya ajira katika ofisi hiyo analazimika kuingia kwenye mahusiano pasipo hiari yake isipokuwa ni kwa sababu tu ajipatie chochote ili mkono uende kinywani.
Jambo linalokua kikwazo sana kwa wanawake walio wengi ambapo hiki ni kitendo cha ukatili wa kijinsia ambapo wengi wanaokumbwa na jambo hili huathirika kisaikolojia kupatana sonona kujiona ni watu wasiofaa ndani ya jamii na pia ni kikwazo cha maendeleo kwa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla wake
Kwa maana hiyo elimu itolewe kwa jamii kuhusu athari zinazoweza kutokana na ukatili huo unaofanywa na viongozi wa taasisi Na maeneo tofauti tofauti ya kazi.
Pia kuihimiza jamii kwamba kujitambua na kujiheshimu na kuwaheshimu watu wengine ndio msingi bora wa kuishi vyema katika jamii zetu.
Kwakuwa kama hali itaendelea hili linaweza kuongeza idadi ya maambukizi, mimba zisizotarajiwa na hata pia ongezeko la watoto wa mitaani ambapo inakua chanzo kikubwa zaidi cha uharifu na mmonyoko wa maadili katika jamii zetu. Pia, kama ikiwezekana wanaotenda jambo hili waadhibiwe vikali na sheria kali zilizowekwa ili kwamba siku wakirudi uraiani waweze kuzitii sheria na kuwa watekelezaji wa kwanza wa sheria hizo ili wengine waige
Asante.

Upvote
1