Ajira JWTZ

Wakujibwea45

Member
Joined
Oct 8, 2021
Posts
62
Reaction score
52
JWTZ walitoa ajira kama mara 2 hivi lakini hakuna hata moja niliyoona watu wakiitwa kwenye usaili. Ya kwanza kuna ile ambayo walitoa wakasema ni kwa ajili ya watu ambao mkataba wao umeshaisha na wapo majumbani ambayo ilikuwa mwaka jana 2023 mwishoni au mwaka huu 2024 mwanzoni kama sikosei na ya pili ya mwaka huu 2024 wakasema waliomaliza mikataba na wapo uraian,mujibu wa sheria na OP flan sikumbuki vzr ni OP gani?

Sasa swali langu ni kwamba watu huwa wanaitwa kwa kupigiwa simu bila ya kutoa majina mtandaon au njia gani inatumika au labda ni ajira ambazo ziko kimkakati an kisiasa zaidi?
 
Sahau kuhusu kua Soldier.
Unajua nilijaribu kufanya uchunguzi binafsi kabla ya kuingia ktk Biashara,
Mfumo wa Ajira unaitaji Connection.
Na ktk Jeshi ndo usiseme bila Connection utoboi, utaenda kusota uko na kazi haupati.
Soma vizuri au wasikilize Vizuri wanakuambia Kabisa kua hawatoi ajira we unaenda kujitolea.
zingatia point kujitolea sio kupata Ajira.
Mi Binafsi ninavyoona ni mtazamo wangu Jeshi ni kazi kama kazi nyingine neno " UZALENDO" Limewekwa kisiasa zaidi kama hauna ndugu Jeshini kazi ya Jeshi/ Uniform zaJeshi utaishia kuziona kwenye TV, au kuona watu walio na ndugu zao ktk vyombo vya usalama wamevaa gwanda.
Jipambanie Kivingine usipoteze mda wako, hizo kazi zinawenyewe.
Tafuta ridhiki upande mwingine
 
Shukrani, nimekuelewa na uliyoyasema nayajua vizuri tu ila bado hujajibu nilichouliza. Nilitaka kujua kama watu walioapply wameitwa kwenda kweny kozi na km ndo ivyo basi hakuna usaili na kama washaitwa njia gani imetumika labda kupigiwa simu direct au vipi na km kuna mtu anajua mtu flan yupo kozi kupitia izo ajira basi atujuze ili tujue na kama ndo kimya basi tujue ni kazi za kisiasa zilizo na lengo la kupumbaza watu kujua kuwa ajira zinatoka kumbe ajira hewa
 
Nafikiri ndio Jsshi lenye mfumo CURRUPT katika kuajiri kuliko yote!!
 
Endelea kusubiri atakupa connection.

Jeshini kuna kitu kinaitwa Baba kanituma[simu toka makao] sasa sijui wewe utawaambia maafande mungu kanituma ?!.
🀣🀣🀣🀣🀣🀣
 
Endelea kusubiri atakupa connection.

Jeshini kuna kitu kinaitwa Baba kanituma[simu toka makao] sasa sijui wewe utawaambia maafande mungu kanituma ?!.
Wote walioajiriwa ni Baba kanituma sio
 
Huko wanaajiriwa ndugu zao
 
Endelea kusubiri atakupa connection.

Jeshini kuna kitu kinaitwa Baba kanituma[simu toka makao] sasa sijui wewe utawaambia maafande mungu kanituma ?!.
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…