SoC01 Ajira kwa vijana kuna haja ya kurejea tulipokosea

SoC01 Ajira kwa vijana kuna haja ya kurejea tulipokosea

Stories of Change - 2021 Competition

Ngosha Mashine

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
665
Reaction score
1,360
Habari wana jukwaa wa jukwaa la story of changes, naomba tuzungumzie suara hili la ajira kwa vijana wa nyanja zote (wasomi na wasiosoma)

Kwa tafsiri fupi ajira ni kazi yoyote isiyo vunja taratibu na sheria inayomuingizia mtu kipato, kama kichwa cha thread kinavyojieleza kuna haja ya kurejea tulipokosea

Maanaake kuna tatizo hapa, basi hebu ngoja tulizungumzie hili tatizo tatizo kubwa ni vijana kushindwa kuzitafsiri ajira ni zipi na hata wakizitafsiri wanazibagua

Nadhani ubaguzi huu umekuwepo kutokana na jamii kujijengea picha kuwa mtu wa aina fulani hatakiwi kufanya jambo fulani mfano, mtu aliyesoma akawa mwanasheria au mhandisi akionekana eti hatakiwi kulima kufanya biashara ndogo ndogo na vitu vya aina hiyo

Kwanini tatizo ni jamii;
Jamii imewajengea picha wanaosoma kuwa wanafaa kukaa maofisini wakiwa wamenawili na sio kufanya kazi za jasho, jaribu kukumbuka wewe wewe ambae miaka hiyo wazazi soma uje kuishi vizuri

Wale ambao kipindi hicho walikuwa wanalima shambani, vibarua mtaani walikuwa wanasemwa wazi wazi kabisa kuwa "unamuona fulani anavyohangaika hakusoma na wewe chezea shule sasa"

Hapa tulipanda mbegu mbaya sana kwa kizazi hiki kwanza tuliwaaminisha kazi za vibarua mtaani, kulima mashambani na kujiajiri ni kazi za mateso hazifai

Nadhani kosa tumeshalijua, sasa tujue tunatokaje hapa

*Kwanza itabidi tuwaandae vijana kufanya kazi yoyote sio za maofisini tu, hapa itabidi kuanzia mashuleni na vyuo kilimo ufundi na biashara

*Tutoe fikra na mawazo kwamba mtu fulani hatakiwi kufanya kazi fulani, hapa pia tutakuwa tumewasaidia na wale wasiosoma maana wao pia wanaonekana wanafanya hizo walizonazo kwa sababu hawakusoma na ni kazi za mateso

Mpaka hapo tutakuwa tumeokoa jahazi maana ajira zipo tatizo ni tafsiri tu iliyopo kwa jamii, ahsante kwa kushiriki na mimi

Ngosha Mashine
 
Upvote 1
Back
Top Bottom